Wakuu wa mikoa mitano ya Burundi inayopakana na Tanzania wamewataka wakimbizi wa nchi hiyo wanaohifadhiwa katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kurudi nyumbani kwao, na kusaidiana na raia wengine wa nchi hiyo ili kuijenga Burundi baada ya vita ya muda mrefu.
kambi ya wakimbizi
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa wakuu hao wa mikoa ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Makamba mheshimiwa Francoise Ngozirazana baada ya mkutano wa ujirani mwema kati ya viongozi wa mikoa ya Burundi na Tanzania, na kwamba Burundi imeweka mazingira mazuri kuhakikisha wakimbizi hao wanapewa huduma stahiki.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema zaidi ya wakimbizi 1500, wamerejea Burundi tangu Januari mwaka huu na wamekuwa na programu ya kuwatoa kambini na kuwapeleka kuona hali halisi ili kushawishi wakimbizi zaidi kurudi Burundi kwa hiari.
Kwa upande wake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma Novati Dauson, akizungumzia suala la kudhibiti raia wa Burundi kuingia nchini kiholela wamekubaliana kuwepo kwa utaratibu wa kuwapa vibali maalum ambavyo vitawawezesha kuingia nchini bila Usumbufu.
No comments:
Post a Comment