Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ameliagiza Jeshi la Polisi na Baraza la Taifa na usalama barabarani kuhakikisha wanayakamata mabasi yote yasiyo na vidhibiti mwendo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
Masauni amesema hayo wakati akizindua baraza la Taifa la Usalama Barabarani makao makuu Dodoma, ambapo amesema miongoni mwa vyanzo vya ajali nchini ni mwendo kasi unaosababishwa na madereva wazembe wasiofuata sheria za usalama barabarani kitendo kinachopelekea ajali nyingi hapa nchini
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jamanne Sagini amesema Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwa kushirikiana na baraza la kazi litaendelea kutoa mafunzo ya usalama barabarani kwa viongozi wa umma wakiwemo makatibu wakuu na wabunge ili kuwajengea uwezo wa kukemea matukio ambayo yanapelekea ajali kutokea.
Aidha Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafugwa, amesema kuwa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani toka limeanzishwa kusimamia kamati za mikoa na wilaya umesaidia ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya fedha zilizotokana na ada za ukaguzi wa magari mbalimbali.
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment