Vikundi vya wananchi wachochea maendeleo katika jamii (WARAGHBISHI) vimesema kuwa vikundi hivyo vimekuwa msaada mkubwa wa kubaini changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii zinazopaswa kutatuliwa na serikali kwa ajili ya kusogeza huduma kwa wananchi.
ERICK FELINO NA PASCHAL MALULU-HUHESO DIGITAL DAR ES SALAAM
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 05, 2022 katika Tamasha la Waraghbishi linalofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa APC Bunju kwa muda wa siku tatu kuanzia leo Oktoba 05-07, 2022.
Washiriki wa Tamasha hilo ambao ni wananchi kutoka Mikoa saba ya Dar es salaam, Simiyu, Kigoma, Shinyanga, Mtwara, Tanga na Geita wakiwa jumla ya washiriki 180 waliohudhuria Tamasha hilo.
Akiwasilisha taarifa ya kundi la Waraghbishi kutoka Wilaya Bariadi mkoani Simiyu, Daniel Peter amesema kuwa wamekuwa wafuatiliaji wakaribu wa miradi inayotekelezwa pamoja na kuibua baadhi ya mahitaji ikiwemo Shule, Afya na Maji.
Hasani Charle ambaye anatokea kikundi cha Waraghbishi kutoka mkoani Mtwara amesema licha ya vikundi hivyo kuanzishwa ili kuchochea maendeleo kwenye jamii wanaiomba serikali kuvindolea vikwazo vikundi hivyo wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.
Amesema kuna baadhi ya changamoto wamekuwa wakiziibua pindi wanapozipeleka kwenye ngazi husika wamekuwa hawatambuliwi kitu ambacho kinakwamisha shughuli za maendeleo.
Nae Ramahan Aman ambaye ni mwana Waraghbishi kutoka Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga amesema kila mwananchi anaowajibu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo kwenye eneo lake hivyo wao wanatumika kama vichocheo ili kuikumbusha serikali ili kufikisha huduma inayolengwa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya mikakati na utafiti kutoka Shirika la TWAWEZA, Baruan Mshale amesema wananchi wote waliopo katika vikundi vya Waraghbishi wajikite katika kuibua changamoto za kimaendeleo kwenye maeneo yao na sio kugeuka wahamasishaji ili kuleta maendeleo kwenye maeneo yao.
Amesema lengo la vikundi hivyo ni kuhakikisha vinasaidia kuondoa mitazamo kwa wananchi ya kuwa tegemezi kwa kila kitu huku baadhi ya miradi ya kimaendeleo inaweza kutatuliwa na wananchi wenyewe wa eneo husika kwa kushirikiana na uongozi wa serikal ya eneo lao.
Kikundi cha WARAGHBISHI kutoka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wakiwa katika majadiliano katika ukumbi wa mikutano wa APC Dar es salaam linapofanyika Tamasha la WARAGHBISHI lililoandaliwa na shirika la TWAWEZA.
WARAGHBISHI kutoka Mbogwe mkoani Geita wakiwa katika majailiano katika ukumbi wa mikutano wa APC Dar es salaam linapofanyika Tamasha la WARAGHBISHI lililoandaliwa na shirika la TWAWEZA.
WARAGHBISHI kutoka Mkoa wa Lindi wakiwa katika majadiliano katika ukumbi wa mikutano wa APC Dar es salaam linapofanyika Tamasha la WARAGHBISHI lililoandaliwa na shirika la TWAWEZA.
WARAGHBISHI kutoka mkoani Mtwara wakiwa katika majadiliano katika ukumbi wa mikutano wa APC Dar es salaam linapofanyika Tamasha la WARAGHBISHI lililoandaliwa na shirika la TWAWEZA.
WARAGHBISHI kutoka wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wakiwa katika majadiliano katika ukumbi wa mikutano wa APC Dar es salaam linapofanyika Tamasha la WARAGHBISHI lililoandaliwa na shirika la TWAWEZA.
WARAGHBISHI kutoka mkoani Kigoma wakiwa katika majadiliano katika ukumbi wa mikutano wa APC Dar es salaam linapofanyika Tamasha la WARAGHBISHI lililoandaliwa na shirika la TWAWEZA.
WARAGHBISHI kutoka wilaya ya Pangani mkoani Tanga wakiwa katika majadiliano katika ukumbi wa mikutano wa APC Dar es salaam linapofanyika Tamasha la WARAGHBISHI lililoandaliwa na shirika la TWAWEZA.
No comments:
Post a Comment