WANAOAMINI UKEKETAJI MKOA WA MARA KUKAMATWA JESHI LA POLISI LAJIPANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 28 October 2022

WANAOAMINI UKEKETAJI MKOA WA MARA KUKAMATWA JESHI LA POLISI LAJIPANGA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime, Rorya limesema kuwa limejipanga kwa ajili ya kuchukua hatua kali dhidi ya wananchi watakaojiusisha na suala la ukeketaji kwa wasichana.

Afisa Ushirikishwaji Jamii Tarime Rorya, SP Daud Ibrahim


Jeshi la Polisi limebainisha kuwa viashiria vimeanza kuonekana kutokana na Mwaka 2022 ni mwaka unaogawanyika kwa mbili, unaoaminika kimila kwa kabila la wakurya kuwa ndio mwaka wa baraka katika suala la ukeketaji katika jamii ya wakurya mkoani Mara.


Afisa wa Polisi upande wa ushirikishwaji Jamii SP Daud Ibrahimu katika kikao cha pamoja kilichofanyika Wilayani Tarime na kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa hapa nchini na wengine kutoka nchi jirani ya Kenya kwa lengo la kuweka mikakati ya kukabiliana na msimu huo wa ukeketaji ambao unasubiriwa kuanza pale shule zitakapo fungwa.


Upendo Kiswaga ni Afisa tarafa ya Ichugu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Kanali Michael Mntnjele anasisitiza suala la ushirikiano baina ya Nchi hizo mbili ili kutokomeza ukeketaji ambao umekuwa ukifanyika hapa nchini.


Aidha maofisa wa serikali kutoka nchi jirani ya Kenya nao wanasisitiza suala la ushirikiano hususani maeneo ya mipakani ili kutokomeza ukeketaji.


Kabila la kurya limekuwa likiamini katika mila ya ukeketaji na ndoa za utoto kwa watoto wa kile kwa kile kinachodaiwa kuwa mtoto wa kike ambae hajakeketwa katika kabila hilo anakuwa na mkikosi hivyo ili kuondoa mikosi hiyo ni lazima mtoto huyo wa kike akeketwe ndipo aolewe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso