Timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu 'Tembo Warriors' itarajia kushuka uwanjani kwenye uwanja wa TFF Riva jijini Instanbul kumenyana na Haiti ikiwa ni mchezo wa hatua ya robo fainali ya mashindano ya kombe la Dunia yanayoendelea nchini Uturuki.
Kikosi cha Tembo Warriors leo Oktoba 5, 2022 kimeendelea kuishangaza dunia kwa kuibamiza vibaya timu kali ya Japan katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa ulemavu yanayoendelea nchini Uturuki.
Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini, Mhe Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wake Dkt. Hassan Abbasi ameongoza kutoa hamasa na mikakati ya ushindi huo wakiungana na watanzania waishio Uturuki.
“Rais na Serikali yenu ipo pamoja na nyinyi, endeleeni kulipigania Taifa lenu, onesheni uzalendo na kuhakikisha mnarudi na kombe nchini na hiyo itakuwa ni zawadi kwa Rais wenu mpendwa na watanzania wote kwa ujumla ”’ amefafanua Mhe. Mchengerwa.
Pia, ameendelea kusisitiza kuwa ahadi zawadi nono kwa timu hiyo ikiwemo shilingi milioni 40 endapo watafuzu robo fainali, shilingi milioni 80 wakifuzu kucheza nusu fainali na shilingi milioni 100 wakifanikiwa kufuzu fainali za michuano hiyo ipo palepale.
Tanzania imefika hatua hiyo baada ya kumaliza nafasi ya tatu hatua ya makundi wakiwa na jumla ya alama nne kisha wakaitoa Japan katika hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment