Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawashirikia watu 13 kwa tuhuma ya kuhujumu na kuharibu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania kati yao wakiwemo watumishi wawili na vishoka wanne pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini wawili.
Na Patrick Mabula , Kahama.
Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa jeshi la polisi wa mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi leo ijumaa kwa waandishi wa habari katika kituo cha polisi cha wilaya ya Kahama alisema watu hao wanatuhumiwa kuhujumu miundombinu ya shirika ikiwemo kujiunganishia umeme kinyume cha utaratibu.
Kamanda Magomi alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na shirika la umeme Tanesco lilifanya oparesheni maalumu kwa lengo la kufichua vitendo vya kihalifu vinavyohusu uhujumu wa miundombinu na liliweze kubaini na kuwakamata watu 13 kati ya hao 7 ni wateja wa shirika hilo.
Alisema watu hao wanatuhumiwa kujiunganishia umeme kinyume cha sheria kwa kushirikiana na watumishi wa Tanesco wasikuwa waaminifu pamoja na vishoka wapatao na kundelea kutumia bila kulipia malipo yeyote.
Kamanda Magomi alisema katika oparesheni hiyo ilibainika watumishi wawili wasiokuwa wa aminifu kwa kushirikiana na waliodaiwa ni vishoka 4 walibainika kuhujumu miundombinu ya shirika kwa kuiba vifaa na kuwaunganishia wateja umeme bila kufaata taratibu kwa maslahi binafsi.
Alisema imebainika kuwa jumla ya Transfoma 73 za umeme zimehujumiwa kwa kuibiwa vifaa mbalimbali na kusasabisha uharibifu na kulitia hasala shirika kwa zaidi ya shilingi milioni 10 kutokana hujuma hiyo iliyokuwa inafanywa na watuhumiwa pamoja na waliounganishiwa na kutumia umeme bule bila kulipa.
Kaimu meneja wa shirika la Tanesco wa wilaya ya Kahama, Mhandisi Tumaini Chonya akifafanua kuhusu hujuma hiyo alisema baadhi ya wafanyakazi wasiokuwa waaminifu walikuwa wanaiba vifaa na kwenda kuwafungia umeme wateja yakiwemo makanisa ya madhehebu ya dini na kutumia umeme bule.
Mhandisi Choya alisema hujuma iliyofanywa na watu hao ni kubwa sana kwa sababu wamelitia hasala shirika na kukwamisha jitihada za kupanua huduma kwa wateja ambapo ametoa wito kwa wananchi kuwa na moyo wa kutoa taarifa kwa Tanesco na jeshi la polisi juu ya vitendo vya hujuma ya miundo mbinu yake.
Aidha Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na shirika la umeme Tanesco linatoa wito kwa mwananchi yeyote anayeju kuwa amaunganishiwa umeme kwa njia zisizo halali na kwamba anatumia umeme bure bila kulipia bili kujisalimisha kwa ofisi ya Tanesco kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa ikiwemo kukamatwa.
Mwisho.
PICHA CHINI.
No comments:
Post a Comment