SERIKALI YAOMBWA KUINGIZA MCHEZO WA KUBETI VYUONI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 19 October 2022

SERIKALI YAOMBWA KUINGIZA MCHEZO WA KUBETI VYUONI


Mkaguzi mkuu wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT) Emmanuel Ndaki, imeiomba serikali kutoa miongozo kwa taasisi za elimu ya juu nchini ya kuanzisha kozi ya michezo ya kubahatisha, kutokana na sekta hiyo kukua kwa kasi



Amesema kwa kipindi cha mwaka 2021-2022 imechangia kwa asilimia 18 katika mapato


Ombi hilo amelitoa katika mafunzo ya kujengea uwezo mameneja wa mikoa yote nchini na wasaidizi wake wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA yanayofanyika jijini Arusha.


Mkaguzi Mkuu wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Emmanuel Ndaki anabainisha kuwa michezo hiyo ina umuhimu katika uchumi wa nchi hivyo serikali inaweza kutoa miongozo ya kutolewa elimu zaidi ili kuzalisha wataalamu wengi katika sekta hiyo.


Nae kaimu meneja makusanyo yasiyo ya kodi idara ya kodi za ndani TRA Joseph Amandus ameeleza kuwa uelewa, na wakusanyaji wa kodi katika mchezo huo ulikuwa mdogo hivyo baada ya mafunzo wanatarajia kupata mapato zaidi


Baadhi ya washiriki wanaopatiwa mafunzo hayo ya siku sita wanaona yamekuja kwa wakati sahihi kwani hapo nyuma walikuwa wanapata ugumu katika ukusanyaji wa kodi .


July 2017 mamlaka ya mapato Tanzania TRA ilipewa mamalaka ya kukusanya kodi katika michezo ya kubahatisha Tanzania bara na inasimamia zaidi ya michezo saba ya kubahatisha.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso