RISH SUNAK ATARAJIWA KUWA WAZIRI MKUU UINGEREZA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 24 October 2022

RISH SUNAK ATARAJIWA KUWA WAZIRI MKUU UINGEREZA


Nchini Uingereza aliyewahi kuwa waziri wa fedha Rishi Sunak anatajwa kujiandaa kuwa Waziri Mkuu mpya nchini humo baada ya Borris Johnson kujiondoa katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo.


Mgombea wa kiti cha Waziri Mkuu Uingereza Rishi Sunak


Bwana Rishi atarithi changamoto zilioonekana kuwa nzito kwa Liz Truss aliyejiuzulu naasi hiyo, ikihusisha changamoto ya kupanda kwa bei, ufinyu wa fedha za umma na kundi la vyama vya upinzani vikisema havina uhalali wa uchaguzi.


Waziri Mkuu wa zamani Borris Johnson wakati akijaribu kugombea kwa awamu nyingine aliungwa mkono na wabunge 102 lakini alishindwa kumshawishi Sunak na mwenzake Penny Mordaunt kuja pamoja kwa masilahi ya taifa.


Rishi Sunak aliye na miaka 42, amewahi kuwa waziri wa fedha ana nafasi nzuri ya kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza na atachukua nafasi ya Truss aliyelazimika kujiuzulu baada ya sera zake za kiuchumi kusababisha wasiwasi katika masoko ya fedha.


CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso