RAIS SAMIA ASAIDIA WALIOJIFUNGUA WATOTO NJITI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 18 October 2022

RAIS SAMIA ASAIDIA WALIOJIFUNGUA WATOTO NJITI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki mekabidhi msaada wa mahitaji muhimu kwa mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni, Kigoma, ujuwa ni msaada kutoka kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan


Rais samia leo tarehe 18 Oktoba, 2022 ameweka jiwe la Msingi katika Jengo la kutolea Huduma za Wagonjwa wa Dharura (EMD) na Wagonjwa wa uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma


“Rais Samia amewashika mkono Mama waliojifungua Watoto njiti kwa kutoa Mashuka, blanket, Vitenge, Sabuni, pampasi, mafuta ya nywele na mahaitaji mengine ikiwa ni pamoja ba vyakula kama Mchele na Sukari” Amesema Waziri Kairuki.


Kwa upende wake, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali italeta Vifaa tiba kwa ajili ya kuhudumia Watoto njiti ikiwa ni pamoja na Mashine za Kufua hewa ya Oksijeni, Mashine za Kuzalisha hewa joto na Mashine za kutunza Watoto njiti.


Naye, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni, Dkt. Stanley Binagi amesema vifaa tiba na Mahitaji hayo yatasaidia utoaji wa huduma bora kwa Watoto Njiti waliopo na wanaoendelea kuzaliwa katika Hospitali hiyo.


Akitoa shukrani zake, Mama wa Mtoto Njiti, Bi. Halima Matayo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za Afya nchini hasa wa Wakina Mama, na kwa kutoa zawadi ambazo zitawasaidia katika kuwahudumia na kuwalea Watoto wao.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso