Richard Mabala, mshauri mwelekezi kutoka shirika la TAMASHA
NA PASCHAL MALULU-HUHESO DIGITAL-DAR ES SALAAM
MSHAURI mwelekezi kutoka shirika lisilo la kiserikali TAMASHA, Richard Mabala amewataka wananchi wachochea maendeleo (WARAGHBISHI) kutokufanya kazi kwa mihemko hali itakayosaidia kutimiza lengo lililokusudiwa katika jamii.
Ametoa wito huo leo Oktoba 06, 2022 katika siku ya pili ya Tamasha la Waraghbishi linafanyika katika ukumbi wa mikutano wa APC jijini Dar es salaam.
Bwana Mabala amesema mtu anaefanya shughuli ya Uraghbishi hapaswi kuwa na mhemko wa namna yoyote kwani yeye ndio anapaswa kuchochea au kuibua maswali kutoka kwa wananchi kwenda kwa viongozi ili kupata suluhisho la mradi lengwa kwa ajili ya maendeleo kwenye jamii.
Pia mtu au watu ambao wanajishughulisha na Uraghbishi hawapaswi kufanya shughuli za Kaya kwa Kaya au Nyumba kwa nyumba bali wanafanya kazi na wananchi au jamii bega kwa bega kwani uraghabishi ni shughuli inayolenga kuibua changamoto zilizopo kwenye maeneo ili kuisaidia serikali kupeleka huduma.
Tamasha la Waraghbishi limewakutanisha zaidi ya wananchi wachochea maendeleo 180 kutoka mikoa nane ya Kigoma, Shinyanga, Tanga, Lindi, Mtwara, Geita, Simiyu na Dar es salaam ambalo limeandaliwa na shirika la TWAWEZA Tanzania kwa mashirikiano na Foundation for civil society, Media Cancelly of Tanzania, mtandao wa jinsia TGNP, TAMASHA na Redio Jamii linalofanyika kwa siku tatu Oktoba 05-07, 2022.
Muwezeshaji Aidan Eyakuze kutoka shirika la TWAWEZA Tanzania akizungumza na Waraghbishi kuhusu changamoto mbalimbali za kukabiliana nazo kwenye utekelezaji wa majukumu ya uraghbishi.
Waraghbishi kutoka mikoa ya Geita na Shinyanga wakifuatilia mjadala kwenye Tamasha la Waraghbishi linaloendelea katika ukumbi wa APC Dar es salaam
Waraghbishi kutoka wilaya ya Pangani mkoani Tanga wakipongeza wasilisho kutoka kwa mwezeshaji katika Tamasha la Waraghbishi linaloendelea katika ukumbi wa APC Dar es salaam
PICHA ZOTE NA ERICK FELINO-HUHESO DIGITAL-DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment