MWENGE wa Uhuru umekamilisha mbio zake wilayani Missenyi mkoani Kagera, ambapo miradi minne ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 932.1 imekaguliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2022,Sahili Nyanzabara Geraruma,ambaye ameridhishwa na utekelezaji wake na hivyo kuizindua,huku akitoa ushauri kwa dosari ndogo ndogo ambazo zimebainika,kurekebishwa mara moja.
NA MUTAYOBA ARBOGAST-HUHESO DIGITAL-BUKOBA
Kiongozi wa mbio za mwenge akikiri kumaliza salama katika wilaya ya Kyerwa,wakati ukiingia wilaya ya Missenyi
Miradi ambayo imekaguliwa na kuzinduliwa ni Mradi wa Maji wa Byamutemba-Byeju, wenye thamani ya sh. milioni 512.5, utakaowanufaisha wananchi 11;983 katika kata ya Nsunga,ambapo kiongozi wa mwenge ameagiza mtu aliyetoa ardhi yake kupisha mradi huo,aunganishiwe maji bure na asitozwe gharama za kumfungia maji,na pia akawahimiza wananchi wanaopitiwa ba mradi huo,licha ya kwamba maji yapo ndani ya mita mia nne,wajitahidi kuvuta maji majumbani ili ndoto ya kumtua mama ndoo kichwani iweze kutimia hasa.
Mwenge umetembelea na kuizindua vyumba viwili vya madarasa vilivyojdngwa kwa nguvu za wananchi na serikali kuu kwa gharama ya sh.40,600,000/- wananchi wakiwa wamechangia sh.600,000 na serikali kuu kutoka mfuko wa Covid-19,ikichangia sh 400,000,000/-
Mradi mwingine ni wa Barabara ya Mabuye Itara yenye urefu wa kilometa 4 inayojengwa kwa kiwango cha changarawe,kipande kilichokamilika kujengwa kina mrefu wa km 2.4 kwa gharama ya sh.288,65,000/-
Kilngozi wa mbio za mwenge,Sahili Geraruma(mwenye skafu)akiwa katika picha pamoja na vijana wa vijana wa hamasa(kulia kwake mwenye shati nyeusi ni mwenyekiti wa vijana wa wilaya Kelvin P.Nazari
Mbunge wa jimbo la Nkenge Florent Kyombo amesema Jimbo linajivunia na kuishukuru serikali kwa kutoa fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa 63 na ujenzi wa hospitali ya wilaya na kituo cha Afya Kanyigo.
Taarifa ya wilaya umesema pamoja na mambo mengine,imeshiriki vizuri zoezi la Sensa ya watu na makazi 2022, kwa asilimia126.10, kwa kuzifikia kaya 66,298,zaidi kuliko kaya zilizokisiwa ambazo ni 51,379,huku majengo yaliyohesabiwa yakiwa 58,232.
No comments:
Post a Comment