Jalala la Wilika mkoani Tabora
Mwanamke mmoja ambaye hajajulikana, anadaiwa kutoa mimba inayokadiriwa kuwa na miezi mitano hadi sita na kisha kukitupa kiumbe alichokuwa nacho tumboni katika dampo la Wilika, Kata ya Gongoni Manispaa ya Tabora, mkoani Tabora, usiku wa kuamkia leo.
Mmoja wa mashuda ambaye amekuwa na kawaida ya kuendesha shughuli zake za kuokota chupa za plastiki kila siku mapema asubuhi, amesema baada ya kufika eneo hilo alitatanishwa na aina ya mfuko mpya ambao ulionekana ukiwa umefungwa kifurushi.
Kufuatia tukio hilo Jeshi la Zimamoto mkoani humo, likawaasa wanawake kutokuwa na mioyo migumu inayopelekea hatua za wao kutupa watoto jalalani.
CHANZO: EATV
No comments:
Post a Comment