Mahakama ya Rufani Tanzania imethibitisha kifungo cha maisha jela alichohukumiwa mwanamke mkazi wa Morogoro mjini, Shani Suleiman (35) kwa kosa la kumbaka mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12.
Ushahidi unaonyesha mwanamke huyo alimbaka mtoto huyo wa kime bila ridhaa yake kwa miaka mitatu kuanzia 2016 mpaka 2019.
Mahakama imeambiwa, wakati wa wa kuanzi kwa vitendo hivyo, mtoto alikuwa na umri wa miaka 12, akisoma darasa la tatu, na liendelea mpaka alipofikisha darasa la tano, mshatikiwa alipokamatwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, ushahidi unaonyesha mwanamke huyo alikamatwa baada ya mama mzazi wa mtoto huyo, akiwa na rafiki yake, kuandaa mtego katika nyumba ya mwanamke huyo ambapo walirekodi tukio hilo kwa kutumia simu janja.
Walifanya uamuzi huo baada ya mtoto kumweleza mama yake kuwa mama Shani, maarufu kama Mama Shafii amekuwa akimwambia amwingilie mara kwa mara na wakati mwingine kinyume cha maumbile na mchezo huo aliufanya kwa miaka mitatu hadi mwaka 2019.
Mwaka 2019 Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro, Ilimuhukumu maisha mwanamke huyo, ambaye alikata rufaa Mahakama kuu, iliyotulipia mbali rufaa yake Julai 28, 2021.
Akakata rufaa ya pili katika Mahakama ya Rufani, ambayo ni ya mwisho kimaamuzi kwa sheria za Tanzania, ambapo sasa imethibitisha hukumu hiyo ya kifungo cha maisha.
Chanzo: bbc
No comments:
Post a Comment