MWANAFUNZI AUAWA KABLA YA MTIHANI WA DARASA LA SABA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 6 October 2022

MWANAFUNZI AUAWA KABLA YA MTIHANI WA DARASA LA SABA

 
 
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, linawashikiliwa watu wawili kwa tuhuma za mauaji wa mwanafunzi wa shule ya msingi Mtumba, Farida Makuya (16).


Mwanafunzi huyo aliuawa usiku wa juzi Jumanne, Oktoba 4, 2022 nyumbani kwao Mtumba jijini Dodoma na watu wasiojulika. 
 


Inadaiwa alipigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akifanya biashara katika klabu cha pombe.



Farida alitakiwa kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi iliyoanza jana na kutarajiwa kumalizika leo Alhamisi ambapo mwili wake ulizikwa jana katika makaburi ya Mtumba na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji la Dodoma. 
 


Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma (RPC), Martin Otieno amesema hadi leo Alhamisi Oktoba 6, 2022, jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa mahojiano lakini msako zaidi unafanyika. 
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso