Mkazi wa Kijijii cha Namanjele mkoani Mtwara, Somoe Mohamed amemchoma mikono mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano kwa madai ya kudokoa mboga na kuiba Sh250.
Akizungumza kijijini hapo Oktoba 4, Somoe amekiri kufanya ukatili huo, akisema lengo lake lilikuwa ni kumwadhibu mtoto kwa tabia mbaya aliyoonyesha.
"Nilikuwa namwadhibu kwa tabia yake. Siku ya kwanza alichukua Sh50 na siku ya pili alichukua Sh200 na baadaye akaanza kudokoa dagaa nikamuonya, lakini hakusikia mpaka sasa mtoto anasiku tatu tangia amechomwa moto,” amesema.
soma zaidi: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/mama-amchoma-mwanaye-mikono-akimtuhumu-kuiba-sh250-3972844
No comments:
Post a Comment