MKUTANO WA MWAKA WA WAKURUGENZI WA AZAKI KUHUSU UWAJIBIKAJI WA FEDHA NA UENDELEVU WA AZAKI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 2 October 2022

MKUTANO WA MWAKA WA WAKURUGENZI WA AZAKI KUHUSU UWAJIBIKAJI WA FEDHA NA UENDELEVU WA AZAKI

Wito umetolewa juu ya Kuachana na kutetea haki za binadamu wanaojihusisha na ndoa za jinsia moja, wito huo umetolea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mh Mwantumu Mahiza alipokuwa akiongea na Wakurugenzi zaidi ya 150 wa Asasi za Kiraia Tanzania ambazo zimekutana kwenye Hotel ya Morena Jijini Dodoma, Mkutano ambao umeandaliwa na Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)


Na Mwandishi wetu - Huheso Digital blog - Dodoma

Mgeni rasmi Mh Mwantumu Mahiza akiongea na Wakurugenzi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakati wakifanya tafakari kuhusu uwajibikaji wa fedha na uendelevu wa Azaki unaofanyika katika hotel ya Morena jijini Dodoma iliyoandaliwa na Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)


Akiongea kwa hisia na kusisitiza Asasi zifuate mila, desturi na tamaduni zetu na uzalendo kama watanzania ili kuondoa mila na desturi ambazo siyo tamaduni zetu ili jamii yetu iweze kuwa bora zaidi na sehemu salama ya kuishi.


Amesema; Wanaume wana akili nyingi kweli, hivi ni kweli ndo akili ya kutaka kuoa mwanaume mwenzio, Wanaume wenyewe kwa wenyewe tunahujumiana, nawasihi tuachane na tabia hii na kama watetezi wa haki za binadamu basi hii isiwe sehemu ya kutetea mambo ambayo yanaharibu mila na desturi zetu kama watanzania.


Amesema; Tuimize kutetea zaidi haki za Watoto, tuimize Elimu, Kilimo cha kisasa, tuimize miradi ya afya, pia akashauri kuwa ni vema kuikosoa serikali kwa hekima na heshima kwani ni muhimu kuwa wazalendo kwa nchi.


Mh Mwantumu ameishukuru THRDC kwa kuandaa mkutano huu wa wakurugenzi ambao wanatoka kila kona ya Tanzania ambapo wanakutana kwa kufanya tafakuri juu ya uwajibikaji na uendelevu wa Asasi za kiraia Tanzania.


Pia Mratibu wa THRDC Ndugu Onesmo Olengulumwa amemshukuru Mh Mwantumu Mahiza kwa kukubali kushiriki Katika mkutano huu, amesema karibu kila mwaka Wakurugenzi ukutana na kufanya tafakuli juu ya shughuli mbalimbali tunazozifanya katika mashirika yetu Tanzania na baadae kuwa na Chakula cha pamoja (Directors dinner) na wakurundenzi wote na kusahau yale ambayo tunakuwa tumeyafanya mwaka mzima na kupunguza stress za maisha.

 

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

PICHA ZOTE NA HUHESO DIGITAL BLOG



Mgeni Rasmi Mh Mwantumu Mahiza alipowasili eneo la Mkutano Morena Hotel na kupokelewa na Mratibu wa THRDC Ndugu Onesmo Olengurumwa, Msajili wa Asasi tanzania Bara Bi Vickness Mayao, Mlajisi wa Asasi Zanzibar Ndugu Ahmed Khalid


Mratibu wa THRDC Ndugu Onesmo Olengulumwa akiongea na Wakurugenzi walioshiriki Mkutano wa tafakuri kuhusu uwajibikaji wa fedha na uendelevu wa Asasi.


Katibu Mkuu wa NACONGO Revocatus Sono akitoa salamu kwa Wakurugenzi waliohudhuria Mkutano ulioandaliwa na THRDC Morena Hotel jijini Dodoma


Mrajisi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Zanzibar Ndugu Ahmed Khalid akitoa Salaam kwa Wakurugenzi waliohudhuria Mkutano ulioandaliwa na THRDC


Msajili wa Asasi Tanzania Bara Bi Vickness Mayao akitoa nasaha zake na kuzungumza na Wakurugenzi walioshiriki Mkutano wa kutafakari juu ya uwajibikaji wa fedha na uendelevu wa Asasi unaofanyika jijini Dodoma ulioandaliwa na THRDC



Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society Ndugu Francis Kiwanga akiongea na kutoa salamu kwa Wakurugenzi walioshiriki Mkutano ulioandaliwa na THRDC jijini Dodoma


Bi Lisa Kagaruki akiwasilisha utafiti mdogo uliofanywa na THRDC kuhusu mfumo wa uwasilishaji taarifa (NGO information Management system) kwa Asasi wakati wa Usajili, utoaji taarifa na kutuma ripoti serikalini, ili kujua faida na changamoto za mfumo huo kwa lengo la kufanyia marekebisho na maboresho yatakayosaidia Mashirika yote kuutumia bila shida yeyote.


Mwenyekiti wa NACONGO Dr Lilian Badi akitoa salamu kwa Wakurugenzi walioshiriki Mkutano ulioandaliwa na THRDC jijini Dodoma


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Tanzania akiwa meza kuu na viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huu wa kuwakutanisha Wakurugenzi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa udhamini wa Tanzania Human Rights defenders Coalition (THRDC)


Baadhi ya Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia wakiwa wanasikiliza kwa makini viongozi mbalimbali walioalikwa kwa ajili ya mkutano wa kujadili uajibikaji na uendelevu wa AZAKI


Mgeni rasmi Mh Mwantumu Mahiza akitoa nasaha zake na kuongea na Wakurugenzi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Tanzania.


Wakurugenzi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakiwa makini kufuatilia mijadala inayoendelea kwenye mkutano huo.


Wakurugenzi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakiwa makini kufuatilia mijadala inayoendelea kwenye mkutano huo.


Picha ya Pamoja Mgeni rasmi pamoja na waratibu wa Kanda wa Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)


Picha ya pamoja Mgeni rasmi pamoja baadhi ya wakurugenzi wa Asasi za Kiraia Tanzania iliyoandaliwa na Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)


Picha ya pamoja Mgeni rasmi pamoja baadhi ya wakurugenzi wa Asasi za Kiraia Tanzania iliyoandaliwa na Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)



Mgeni rasmi Mh Mwantumu Mahiza akizindua kitabu ambacho kinaangazia utafiti mdogo 
uliofanywa na THRDC kuhusu mfumo wa uwasilishaji taarifa (NGO information Management system) kwa Asasi wakati wa Usajili, utoaji taarifa na kutuma ripoti serikalini


Baadhi ya Wakurugenzi wakiwa makini na kushiriki Mkutano wa tafakuri kuhusu uwajibikaji wa fedha na uendelevu wa Asasi katika hoteli ya Morena jijini Dodoma ulioandaliwa na Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso