MENEJA TANROADS MKOA WA SHINYANGA,MHANDISI MIBARA ATOA ZAIDI YA SH.MIL 2 KUBORESHA MIUNDO MBINU SHULE YA MSINGI TOWN - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 21 October 2022

MENEJA TANROADS MKOA WA SHINYANGA,MHANDISI MIBARA ATOA ZAIDI YA SH.MIL 2 KUBORESHA MIUNDO MBINU SHULE YA MSINGI TOWN

Meneja wa wakala wa barabara (Tanroad) mkoa wa Shinyanga,Mhandisi Mibara Ndilimbi,ametoa baadhi ya vifaa vya ujenzi ikiwemo mchanga,saruji na Tofali kwaajili ya ujenzi wa uzio katika shule ya msingi Town hali itakayosaidia kuboresha miundombinu katika Shule hiyo .

Wanafunzi wa Darasa la Saba shule ya msingi Town


NA HALIMA KHOYA - HUHESO BLOG - ,SHINYANGA


Akizungumza katika mahafali ya darasa la saba, shule ya msingi Town, mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyofanyika jana Oktoba 21,2022 katika viwanja vya shule hiyo.


Awali mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Town, Meshaki Helmani,amesoma risala ya shule mbele ya mgeni rasmi na kueleza mafanikio pamoja na changamoto zinazo ikabili shule hiyo yenye zaidi ya wanafunzi elfu moja licha yakwamba Shule hiyo haina uzio hali inayo pelekea baadhi ya vijana kuingia katika vyoo vya wanafunzi wa kike kwa lengo la kuwafanyia vitendo ya ukatili.


"Uvamizi na mwingiliano wa wafanyabiashara na wajasiriamali katika viunga vya shule hali inayopelekea uchafuzi wa mazingira ikiwemo vyoo vya wanafunzi kujaa mara kwa mara.


Akijibu risala iliyosomwa na mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Mhandisi Ndilimbi ambaye ni mgeni rasmi ametoa baadhi ya vifaa vya ujenzi katika shule hiyo ili kupunguza adha ya uchafuzi wa mazingira yanayo ikabili shule hiyo iliyo jengwa toka mwaka 1942 .


Pia Mhandisi Ndilimbi amekabidhi kiasi cha Shilingi milioni moja tasilimu kwa ajili ya ukarabati wa miundo mbinu ya
shule hiyo hali itakayo saidia kuboresha mazingira ya kujifunzi na kufundishia.


Nao baadhi ya wazazi na walezi wanaosomesha watoto wao katika shule hiyo wamemshukuru Mhandisi Ndilimbi kwa kuchangia vifaa vya kukarabati miundombinu ya shule huku wanafunzi wakieleza kuwa iwapo ujenzi wa uzio wa shule hiyo utakamilika utasaidia kuinua kiwango cha taaluma kwao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso