MADIWANI WAMCHARUKIA MENEJA TARURA,WAAHIDI KUTOA USHIRIKIANO UJENZI WA BARABARA,SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 29 October 2022

MADIWANI WAMCHARUKIA MENEJA TARURA,WAAHIDI KUTOA USHIRIKIANO UJENZI WA BARABARA,SHINYANGA

WAKALA wa barabara mjini na vijijini (TARURA) Manispaa ya Shinyanga wameshauriwa kuzingatia Taratibu zote zinazotakiwa katika ujenzi wa Miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Madiwani ili kuondokana na adha la ukosefu wa ushirikiano kati yao na uongozi wa eneo husika.



NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA


Rai hiyo imetolewa jana oktoba 28 2022 katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wakati wakichangia taarifa ya utendaji kazi miradi ya kudumu katika kikao hicho.


Ambapo Madiwani wametoa Rai kwa Idara hiyo akiwemo diwani wa Kata ya Ibinzamata, Ezekieli Sabo,amewataka TARURA kuandika barua kwa viongozi wa eneo husika ambapo mradi huo unafanyika ili watambue na washiriki katika ufuatiliaji wa maendeleo ya miradi hiyo.


Mbali na kutoa Taarifa kwa Viongozi pia Tarura wametakiwa kufuatilia wakandarasi katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha wanafuata taratibu zote za ujenzi na kutoa ushauri kulingana na eneo husika ili kutengeneza miundombinu yenye uimara.


Akipokea taarifa hiyo kutoka kwa Madiwani Kaimu Meneja wa TARURA,Wilaya ya Shinyanga Yohana William, amesema kuwa maelekezo yote waliyopewa na Madiwani watayafanyia kazi huku akiahidi kuanza utekelezaji katika miradi ambayo inatekelezwa katika maeneo mbalimbali katika Manispaa hiyo ikiwemo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara,makaravati, madaraja pamoja na mitaro.


"Suala la wakandarasi ambao wamekuja saivi umetuomba kuzingatia muda na kuweza kumaliza kazi kwa wakati kwaivyo tutalifuatilia ili kukamilisha miradi hii bila kuchelewa"Amesema Wiliam.


"waheshimiwa hapa wametoa maoni kuhusu kutoa taarifa kwa viongozi wa mtaa kwa hilo tutaifanyia kazi na tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na tunaahidi kujirekebisha na tutaleta barua kwa uongozi wa mtaa husika"Ameongeza.


Katika hatua nyingine William amewaomba Madiwani kwa kushirikiana na wananchi wao kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa miundombinu iliyokwisha kujengwa ili kuulinda uimara wa miundombinu hiyo iweze kudumu na kutumia na vizazi vijavyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso