HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI YAIRIDHISHA KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 29 October 2022

HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI YAIRIDHISHA KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera imefanikiwa kuiridhisha Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa(USEMI),kwa kutoa ufafanuzi wa matumizi ya 60% ya Matumizi Mengineyo katika bajeti ya mwak 2021/22,baada ya kuitwa mbele ya Kamati hiyo mjini Dodoma.


NA MUTAYOBA ARBOGAST-HUHESO DIGITAL BLOG


Kikao hicho kimehitimishwa kwa Kamati ya USEMI kuridhika na matumizi ya asilimia 60 ya Matumizi Mengine na kuendelea kuisisitiza Halmashauri kuendelea na juhudi madhubuti ya ukusanyaji mapato ya ndani.


Katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mh Angella Kairuki, Naibu Waziri Na Naibu Katibu Mkuu kimefanyika katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Tanzania Dodoma hjku walioitwa mbele ya Kamati wakiwa ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Missenyi,Waziri Kombo,na wakuu wa idara,msafara ukipngozwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera,Toba Nguvila.


Mbunge wa Jimbo la Nkenge,Florent Kyombo ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali(PAC),kuhakikisha maelezo yanayotolewa na Kamati ya Bunge,akishirikiana na Halmashauri ya wilaya,yanatekelezwa.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso