Mkuu wa Wilaya Shinyanga, Jasinta Mboneko, Amewataka viongozi wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) kuwa wazalendo wakati wa kutekeleza majukumu yao hali itakayosaidia kupunguza malalamiko yanayotolewa na wananchi juu ya Jeshi hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Shinyanga mjini.
NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA.
Amesema hayo leo oktoba 13 mwaka huu wakati wa Kikao cha Kusimika viongozi 6 wa Jeshi la Jadi Tarafa ya Mjini,Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo kilichofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Majira ya Saa 4 asubuhi.
Mhe.Mboneko,Amesema kuwa,Viongozi wa Jadi Maarufu kama Sungusungu waliosimikwa wawe wazalendo katika utendaji wa kazi zao hali itakayosaidia kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kurahisisha mawasiliano mazuri kati yao.
Vilevile Mboneko,Amewataka viongozi hao kufanya kazi bila ya upendeleo wala uonevu hali itakayosaidia kudumisha na kulinda haki za raia kwa manufaa ya jamii.
"Viongozi watakaosimikwa leo hakikisheni ni wazalendo,wenye hofu ya Mungu,wenye kuheshimu wananchi pamoja na kujiheshimu,mwenye kukemea Rushwa na wala asiwe mwenye kujihusisha na makosa yasiyo msingi lakini pia na nyinyi muwape ushirikiano mzuri"Amesema DC Mboneko.
Kwa upande wake Kamanda Mkuu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga,John Kadama amesema kuwa viongozi wa jeshi hilo pamoja na Sungusungu wanapaswa kuacha kuwatoza wananchi faini kubwa kwa makosa madogo hali inayopelekea kuvunjwa kwa taratibu na sheria za Jeshi hilo.
"Kuna sungusungu mnatumia vyeo vyenu vibaya kwasababu kunakua na makosa madogo madogo ambayo ni yakuelekezana ila nyie mnataka mpewe ng'ombe wawili kama faini ya kosa dogo,Msitumie vibaya jina la sungusungu kujipatia kipato"Amesema Kadama.
Nae Mwenyekiti wa Sungusungu Tarafa ya Shinyanga Mjini,Paul Gile,Ameeleza upekee atakaoufanya katika madaraka yake kwa kuwalinda wananchi pamoja na mali zao ikiwa ni kwa kubainisha aina na tabia za watu katika familia zao ili kuwatambua wahalifu katika jamii zinazowazunguka.
pia Paul Gile,Amebainisha sababu ya uwepo wa uhalifu katika jamii amesema,uhalifu unasababishwa na malezi ya wazazi kwa watoto wao kwa kuwaendekeza wanapofanya vitendo visivyofaa hali inayowajengea mazoea hatimae kuingia katika makundi mabaya kwa kuwapora watu vitu,kuwajeruhi pamoja na ubakaji.
No comments:
Post a Comment