SHIRIKA la Mavuno la wilayani Karagwe,lililoanzishwa mwaka 1993,likitekeleza miradi yake katika wilaya za Karagwe na Kyerwa,limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia wananchi adha ya kutopata maji safi na salama,kwani kaya 11,000 kati ya kaya zipatazo 125,242 za wilaya hizo wanapata maji safi na salama kutoka shirika hilo.
Wageni kutoka manispaa ya Furth,Ujerumani wakiwa katika kazi la kitenge,zawadi kutoka shirika la Mavuno(wa tatu kutoka kushoto ni kiongozi wa msafara,Meya mkuu wa mji wa Furth,AndreasHorsche).
Na Mutayoba Arbogast Huheso digital blog Bukoba
Wananchi wengine hupata maji toka vyanzo vingine vikiwemo vya serikali, mashirika, watu binafsi na chemichemi,huku kukiwa bado na uhitaji mkubwa wa maji kuwafikia katika mazingira yao ndani ya mita 400.
Mkurugenzi wa shirika hilo, Charles Bahati, amesema wanazihudumia shule za msingi 131,na makundi ya vijana yapatayo 67 kuhimiza shughuli za ujasiriamali na elimu juu ya VVU/UKIMWI,huku pia shirika hilo likimiliki shule ya sekondari ya Mavuno yenye wanafunzi 399,huku ujenzi wa miundombinu ya kidato cha tano na sita ukiendelea kwa kiwango cha kuridhisha.
Aidha shirika liko mbioni kuanzisha pia shule ya sekondari ya wavulana.
Hayo yamejili katika kikao cha pamoja kati ya shirika hilo na wageni wao kutoka Manispaa ya Furth nchini Ujerumani, ambao wamekuwa wakilifadhili shirika hilo, ili kujionea utekelezaji wa miradi hiyo.
Ujumbe huo wa watu saba umeongozwa na Meya mkuu wa Manispaa hiyo,Andreas Horsche,aliyefuatana pia na Meya mwingine kutoka chama cha upinzani.
Meya Horsche, baada ya kutembelea miradi hiyo,amefurahishwa na utekelezaji wa miradi hiyo,na kuahidi misaada zaidi kwani kila wanachotuma kinatumika kama ilivyopangwa.
Mwenyekiti wa Bodi wa shirika la Mavuno,Angela Anselimi,ameahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa majukumu kwa faida ya wanajamii,huku diwani wa kata ya Chonyonyo, Anord Rwesheleka, ambaye amemwakilisha mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Wallace Mashanda, akiwashukuru wageni hao kuridhia Manispaa ya Furth kuwa pia marafiki wa Halmashauri hiyo.
Hafla hiyo imekolezwa na shamrashamra za kukata keki kusheherekea siku ya kuzaliwa ya mmoja wa wageni hao ambaye amekuwa akitoa msaada mkubwa kwa shirika, Bruda Andreas Richard(69),na baadaye Misa takatifu ambayo imeongozwa na Padre Dachius Kamugisha Kanani.
Wageni na wenyeji katika picha ya pamoja.
Andreas Richard ambaye ametimiza miaka 69 akikata keki kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Baaada ya Misa,kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Mavuno Charles Bahati.
No comments:
Post a Comment