Baadhi ya wananchi wenye Ugonjwa wa macho Mkoani Shinyanga wamemshukuru Mbunge wa Viti maalum Lucy Mayenga, kwa huduma ya Matibabu ya Macho iliyotolewa na Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Free eye camp, iliyowasaidia kuondokana na adha ya uoni hafifu na matatizo ya macho wananchi hao.
Mbunge wa viti maalum Mkoa Shinyanga ,Lucy Mayenga Akizungumzia Juu ya Matibabu ya Macho.
NA HALIMA KHOYA, Huheso Blog - SHINYANGA.
Zoezi la utoaji wa huduma hiyo limeanza alfajiri ya leo, oktoba 14 litakalomalizika tarehe 16 mwaka huu katika chuo cha Shy Com Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo.
Wananchi hao wametoa shukrani zao kwa Mbunge juu ya kupatiwa huduma ya matibabu ya macho huku wakieleza kuwa huduma hizo zitawasaidia kuondokana na changamoto ya kutokuona vizuri sambamba na kubainisha huduma nzuri zinazotolewa na madaktari hao.
Kwa upande wake Mratibu wa Jopo la Madaktari bingwa wa macho kutoka Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania free eye camp,Dkt.Ain-Sharif, Amesema taasisi hiyo imejikita kwenye utoaji wa huduma za kijamii pamoja na huduma ya macho ambapo wanatoa huduma hiyo kwa wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hizo ili kuwanusuru wagonjwa Nchini.
Dkt.Ain-Sharifu,Amesema kuwa, wamekubali kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Lucy mayenga, kuweza kutoa huduma kwa kuwapatia matibabu ya macho kwa takribani watu 3,000-4,000 huku akibainisha kuwa, moja ya huduma zinazotolewa ni pamoja na upasuaji wa macho, kutoa miwani na kutoa dawa kwa wagonjwa hao bila malipo ya aina yoyote.
“Taasisi hii imejikita kwenye utoaji wa huduma za kijamii na huduma za macho,Ni uzoefu wetu kutoa huduma sehemup tupo hapa kwa siku tatu ili kutoa matibabu kwa wagonjwa wenye uhitaji”Amesema Ain-Sharif.
Aidha kwa upande wake Mbunge wa viti maalum Mkoa Shinyanga Lucy Mayenga, Amesema sababu iliyomfanya akaleta waatalamu wa macho katika Mkoa huu ni uwepo wa Wagonjwa wengi wa Macho huku Madaktari bingwa wa ugonjwa huo kuwa wachache hali inayopelekea kuendelea kuwepo kwa waathirika wa mamcho katika Mkoa Shinyanga.
“Kuna changamoto kubwa kwa Mkoa huu kuwa na uchache wa Madaktari bingwa wa macho kwaiyo nimeona vyema mimi kama Mbunge wa Shinyanga kuweza kuwaletea wananchi wote matibabu karibu,pia nawashauri wananchi waweze kupima afya zao pale wanapoona dalili za kuumwa macho ili kuepusha athari za kushindwa kuona sambamba na kuwa na uonihafifu”Amesema Mayenga.
No comments:
Post a Comment