Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Wilaya ya Kahama Bi Aisha Nyemba ametoa wito kwa waajiri kulipa Michango kwa wakati ili kuurahisishia Mfuko huo kuwalipa wanachama wao kwa muda muafaka.
Na Anas Ibrahim - Huheso blog Kahama
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Wilaya ya Kahama Bi Aisha Nyemba akiwa na wanachama pamoja na wafanyakazi wa NSSF kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika ofisi za NSSF Kahama.
Amesema hayo alipokuwa Akizungumza na waandishi wa habari Oct 7, 2022 kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya NSSF ambayo yalianza Oct 3 mwaka huu amesema kuwa waajiri ndiyo wateja wao wakubwa kwa kulipa michango yao kwa wakati
Aidha Nyemba amewashukru wanachama wa NSSF na kuwahimiza waendelee kuwaamini kutokana na huduma zao ambapo mfuko huo unazidi kuboresha mifumo yao
Kwa upande wake Afisa Matekelezo wa NSSF Ndg Shaban Mbwana Amesema kuwa lengo la wiki hii nikutambua umuhimu wa huduma zitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuleta uelewa Kwa wananchi
Hata hivyo wiki ya huduma kwa wateja imeadhimishwa kwa siku tano kuanzia Oct 3 ambapo kilele chake ni leo Oct 7 yenye kauli mbiu isemayo “HUDUMA BORA NI KIPAUMBELE CHETU’’
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Wilaya ya Kahama Bi Aisha Nyemba akimlisha keki Mfanyakazi wa NSSF Ndugu Fredrick Kabalega kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja mjini Kahama
Maandamano ya Wafanyakazi wa NSSF Kahama wakiwa kwenye maandamano katika kilele cha huduma kwa wateja kilichofanyika Kahama
Wafanyakazi wa NSSF walivyoshiriki maandamano kwenye kilele cha huduma kwa wateja mjini Kahama
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Wilaya ya Kahama Bi Aisha Nyemba akikabidhi cheti cha mfanyakazi bora Bertha Mwambe kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja mjini Kahama
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Wilaya ya Kahama Bi Aisha Nyemba akikabidhi cheti cha mfanyakazi bora Magreth Mwaibasa kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja mjini Kahama
PICHA ZOTE NA ANAS IBRAHIM - HUHESO BLOG
ANGALIA VIDEO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment