Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mh. Sophia Mjema amewataka Viongozi kuanzia ngazi ya Wilaya hadi vijiji Mkoani humo kuwa Mabalozi wazuri katika kufikisha elimu kwa Jamii kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa EBOLA huku akitoa tahadhari kuwa ugojwa huo haujafika katika Mkoa wa Shinyanga .
NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA.
Mh Mjema ameyaeleza hayo jana Oktoba 6 wakati wa ufunguzi wa kikao Cha Kamati ya huduma za afya ya msingi Mkoa wa Shinyanga kuhusu kupambana na ugonjwa wa EBOLA sambamba na kusaini mkataba wa utekelezaji wa afua za lishe Mkoani humo.
Mjema, Amewataka viongozi wote kuwa mabalozi wenye kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na Raisi ili kufikia malengo ya serikali hali itakayo uweka mkoa huo sehemu nzuri kitaifa.
RC Mjema akieleza taarifa za ufuatiliaji za ugonjwa huu amesema kuwa Mikoa ailiyopakana na Nchi jirani ya Uganda ipo kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa EBOLA Kutokana na shughuli za kijamii zinazo wakutanisha watu mbali mbali kutoka sehemu tofauti huku akiwataka wananchi wote wachukue tahadhari juu ya ugonjwa huo ili kuuweka salama mkoa walote kwa ujumla.
"Taarifa za ufuatiliaji kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu zinaonyesha Mikoa iliyo mpakani na Nchi jirani ya Uganda ipo kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa EBOLA kutojana na shughuli za kijamii na kiuchumi, tukumbuke na sisi kupitia upande wa kahama bado tuna wafanyabiashara wanaingiliana kwenye shughuli mbali mbali hivyo jukumu letu kama mikoa mingine tuchukue tahadhari"Amesema Mjema.
Pia amesema kuwa Mkoa umeshajipanga kwa kuainisha vituo vya afya vilivyotengwa kwaajili ya dharura ya wagonjwa wa ebola ambavyo ni Hospital ya rufaa ya mwawaza jengo la dharura kwa Manispaa ya Shinyanga, Kituo cha afya kishapu kwa halmashauri ya kishapu, Kituo cha afya Nyasubi kwa Manispaa ya kahama, Hospital ya ushetu jengo la dharura kwa halmashauri ya ushetu, Kituo Cha Afya Bugarama kwa halmashauri ya msalala, pamoja na Hospital ya wilaya Shinyanga kwa halmashauri ya Shinyanga.
Aidha kwa upande wake Mratibu wa magonjwa ya kuambukiza Mkoa Shinyanga,Mussa Makungu, Ameainisha jinsi ugonjwa huo unavyoenea na baadhi ya dalili za awali zinazoashiria mtu aliyepata maambukizi hayo ikiwa ni pamoja na kuwataka wananchi wote kuwa kwa yeyote atakaye patikana na dalili kama hizo awahi kuripoti kituo cha afya kwaajili ya vipimo zaidi.
"Ebola inaambukizwa kwa majimaji yanayotoka kwa mgonjwa mfano,mkojo,jasho,mate, pamoja na kukumbatiana na mgonjwa, lakini pia tunaweza kujikinga ugonjwa huo kwa kunawa mikono kwa maji safi na vitakasa mikono(sanitizer),usafi binafsi na mazingira yanayotuzunguka,na kuacha kusalimiana kwamikono na kukumbatiana pamoja na kula wanyama pori bila vipimo maalumu"Amesema Makungu.
No comments:
Post a Comment