Kijana Mmoja mwenye umri wa miaka 24 Mkazi wa Burugalila Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo, Baraka Mayala Amevamiwa na kujeruhiwa kwa kukatwa na panga sehemu mbali mbali za mwili, kichwani,mkononi pamoja na miguuni na watu wasiofahamika akiwa anautetea uhai wake, watu hao walifanikiwa kumuibia fedha alizokuwa nazo kijana huyo.
NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA
Tukio la kujeruhi limetokea jana Oktoba 07 mwaka huu katika Kijiji cha Bujinge Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Mkoa lni Shinyanga Majira ya saa nne usiku.
Akisimulia Mhanga wa tukio hilo Baraka Mayala amesema watu hao wasiofahamika walimvamia njiani akiwa anatoka kwenye harusi katika kijiji jirani na kutaka kumuibia fedha pamoja na simu aliyokuwa nayo lakini watu hao walifanikiwa kumpora hela pamoja na kumkata na panga katika mwili wake hali iliyopelekea jeraha kubwa katika kichwa chake.
"Watu hao walinivamia njiani na kuanza kunikagua katika mifuko ya suruali na kutaka kuniibia hela na simu lakini nilijitetea kwa kupigana nao ila walifanikiwa kunikata na panga kichwani mara mbili na nilipotaka kukimbia walinikata katika miguu yangu, na nilipotaka kutambaa kwa mikono walinikata mikononi kisha kukimbia na kuniacha bila msaada"Amesema Baraka.
kwa upande wao ndugu wa Kijana huyo wameeleza kuwa tukio hilo ni lakikatili huku wakibainisha kuwa watu wanaofanya matukio hayo ni wale wasio na ajira pia wameiomba serikali kuweka ulinzi na mitego ili kuwakamata watu wanaoshiriki kufanya vitendo hivyo ili kuleta amani katika jamii.
Nae Mwenyekiti wa Mtaa wa Burugalila,Iddy Dotto Amesema kuwa hakupata taarifa juu ya tukio hilo huku akiwashauri wazazi wawe makini kwa vijana wao juu ya suala la kuchelewa kurudi na kuwakanya vijana wao kutoka usiku ili kuepusha adha za kukutana na vibaka wasiofahamika ambao wanaleta maafa katika jamii na kuongeza kuwa ndugu wa kijana huyo walifanikiwa kutoa taarifa Polisi kwaajili ya uchunguzi ili kuwabaini watu hao.
Akithibitisha kumpokea kijana huyo kwa niaba ya Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa Mkoa Shinyanga Dkt.Kambi Buteta, Amesema majira ya alfajiri ya leo alimpokea kijana huyo akiwa na majeraha katika kichwa,miguu pamoja na mikononi huku akiwa anavuja damu nyingi ambapo tulifanikiwa kumpatia matibabu yaliyozuia kutokwa na damu katika majeraha yake.
"Jana alfajiri tulimpokea Baraka Ngassa akiwa na majeraha kichwani,majeraha ambayo yanaashiria alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali lakini tulifanikiwa kumpatia huduma ya kwanza ili kuzuia damu zisiendelee kuvuja ambapo hali ya kijana huyo ni nzuri kiasi na bado anaendelea kupata matibabu zaidi"Alisema Dkt.Buteta
Nae Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi ACP,Leornad Nyandahu amesema Jeshi hilo linaendelea na jitihada za kuwatafuta watuhumiwa walioshiriki kumjeruhi kijana huyo
Kijana akiwa na majeraha ambayo aliyapata baada ya kuvamiwa.
No comments:
Post a Comment