WAZIRI BASHUNGWA AAGIZA KUUNDWA KWA TUME MAALUM YA KUCHUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI KAGERA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 10 September 2022

WAZIRI BASHUNGWA AAGIZA KUUNDWA KWA TUME MAALUM YA KUCHUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI KAGERA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza  Mkuu wa Mkoa Kagera, Mhe. Albert John Chalamila kuunda Tume maalum itakayopokea malalamiko ya   ardhi  yaliyokidhiri katika Halmashauri ya  wilaya ya Karagwe, Mkoani Kagera.


Ametoa agizo hilo leo tarehe 10 Septemba 2022 wakati aliposhiriki kikao cha Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi wilaya karagwe na kupokea malalamiko ya kuibuka vna kukithiri kwa migogoro sugu ya ardhi bndani ya wilaya ya Karagwe.


Amesema Tume hiyo  maalum itafanya kazi ya kufuatilia kwa undani migogoro sugu na inayoendelea  kuibuka ndani ya mkoa Kagera ambayo inachangia uvunjifu wa amani na kuleta umasikini kwa wananchi.


Aidha, Bashungwa amepokea changamoto kuhusu vijana wasiokuwa na Vitambulisho vya NIDA kutopewa Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ambapo Bashungwa amekiri kuwepo kwa changamoto  hiyo ambayo ipo katika mfumo Mpya wa utoaji wa Mikopo katika Halmashauri.


HBashungwa amesema kutokana na changamoto ya upatikanaji wa Vitambulisho vya NIDA katika mikoa ya mipakani, Ofisi ya Rais TAMISEMI itafanya Maboresho ya mfumo huo ili kutoa fursa kwa vijana ambao hawajapata vitambulisho hivyo kunufaika na mikopo hiyo.
 

Wakati huo, Bashungwa ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi Kubwa anayoifanya ya kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na alitumia  nafasi hiyo kumshukuru Rais kwa fedha nyingi za miradi anazoendelea Kuleta Mkoa Kagera. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso