Jumla ya wanafunzi 521 wa Shule mbalimbali wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, wameripotiwa kukimbia masomo kwa kipindi cha miezi miwili sasa hali ambayo imeilazimu Serikali kutangaza mpango wa dharula wa kukabiliana na tatizo hilo
Ni katika kukabiliana na changamoto ya utoro shuleni, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Lupakisyo Andrea Mjukuu wa Kapange, amelazimika kutangaza operesheni ya kuwasaka na kuwarejesha masomoni wanafunzi 521 wanaodaiwa kususa masomo, ikiwa ni pamoja na wazazi wanaohusika kuwaoza au kuwaozesha kukabiliwa na shinikizo la sheria
“ Tumeanzisha operesheni ya kuwasaka watoro wote. Awe mtoto wa kike, awe wa kiume lazima asome kwa sababu Taifa hili linamuhitaji sana. Kila mtoto (mtoro) tutamfikia kwa jina lake na mahala alipo.Tukikuta mtoto hayupo tutamchukuwa mzazi mpaka atakapotuletea mtoto ndipo tutamuachia, pelekeni salamu,” amesema DC Kapange.
Amesema elimu ni takwa la kisheria na mikataba ya Kimataifa, iliyoridhiwa na Tanzania kupitia Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009, hivyo ni lazima watoto wote waelekee masomoni shuleni kwa faida ya maisha yao na Taifa kwa ujumla
“Elimu ni haki ya mtoto, tunataka mtoto apate haki yake. Yaani wilaya nzima watoto 521 (watoro shuleni) wilaya nzima, hii haikubaliki. Na hii ninayozungumza ni kutoka tarehe 1 mwezi wa 7 mpaka tarehe 12 mwezi wa 9, yaani hapa katikati watoto hawaonekani (shuleni) mnataka kuwapekela wapi! Watoto pingeni kuolewa,” amesema DC Kapange
“Tunakuahidi tutafanyakazi kwa ushirikiano kwa sababu wewe unaendelea kutupa ushirikiano mkubwa tunapokuwa na changamoto. Kwa hiyo, tunakuahidi kwamba sisi tunakwenda kufanyakazi,” amesema Isabela.
“Tunajua kuna idadi kubwa sna kule (mgodini) wameacha shule wapo mgodini wanafanyakazi. Lakini, tuna changamoto ya wazazi. Hali duni wazazi wanawazuia watoto kuja shuleni ili wakafanye shughuli za kiuchumi,” amesema Mecklina.
Wakati hayo yakijiri, Mkuu wa Wilaya hii ya Bariadi, Lupakisyo Andrea Mjukuu wa Kapange, amelazimika kufunga safari hadi nyumbani kwa mwanamama mmoja mkazi wa Kata ya Dutwa, anayedaiwa kumzuia mwanaye kwenda shuleni na amemuamuru kumpeleka mtoto huyo masomoni, vinginevyo atakiona cha mtemakuni
“Alikuwa anasoma na alikuwa anafaulu mitihani yake yote na mitihani yake yote ninayo, anafanya vizuri (masomoni). Kama umemjenga kichwani kwamba nenda shuleni maadamu wanalazimisha kwanda shule ukafeli, akifeli (mitihani) nakuweka ndani,” DC Kapange ameonya.
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment