WAHIMIZWA KUENDELEA KUCHANGIA UJENZI HOSTELI SHULE YA SEKONDARI KIKUKWE WILAYANI MISSENYI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 28 September 2022

WAHIMIZWA KUENDELEA KUCHANGIA UJENZI HOSTELI SHULE YA SEKONDARI KIKUKWE WILAYANI MISSENYI

 WANANCHI wa kijiji cha Bugombe,kata ya  Kanyigo,wilayani Missenyi  wamehimizwa kuendelea kuchangia ujenzi wa hosteli ya shule ya sekondari Kikukwe iliyomo katani humo ili kuwanusuru wanafunzi,hasa wa kike,kutokana na adha mbalimbali za njiani wanazokumbana nazo.



Mwenyekiti wa kijiji cha Bugombe,kata ya Kanyigo,Japerson Mutabuzi,akiongea na wanakijiji kuhusu maendeleo ya kijiji hicho( kushoto Kwame ni Afisa kilimo wa kata,Michael Machiya)



Na Mutayoba Arbogast Huheso Digital Blog - Bukoba

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kijiji hicho Japerson Mutabuzi wakati wa mkutano wa hadhara wa dharura kueleza mambo kadhaa muhimu yanayohitaji utekelezaji wa haraka.


Amesema tangu suala la kutangazwa michango ya ujenzi huo mwaka mmoja uliopita,kijiji cha Bugombe kinasuasua katika uchangiaji,huku kijiji jirani cha Kikukwe iliko shule hiyo kikiwa mstari wa mbele kwa uchangiaji.


Mkutano huo umekubaliana kwa kauli moja kuwa,kwa ambao bado hawajatoa michango yao,wafanye hivyo ndani ya wiki mbili,vinginevyo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria


Umoja wa Maendeleo Kikukwe(UMKI),ndio waanzilishi wa ujenzi huo ambao umefika hatua ya kukamilisha msingi kwa kutandika jamvi la zege,huku wanachi wa vijiji vingine katika kata za Kanyigo na Kashenye wakiwaunga mkono.


Shule hiyo ya kata inachukua wanafunzi wa vijiji vya Kikukwe na Bugombe.


Aidha katika mkutano huo wamechaguliwa wajumbe 14 (ke 7,na me 7)watakaokuwa wakiratibu mwenendo wa maendeleo na changamoto kwa walengwa wa mpango wa TASAF kijijini hapo,ambapo kijiji kina wanufaika 35


Kwa mujibu wa Michael Machiya,Afisa kilimo wa kata na mratibu mhamasishaji wa mpango huo katani,kuchaguliwa wajumbe hao ni mpango mpya katika kuhakikisha fedha inayotolewa inakwenda kwenye matumizi sahihi ya kupambana na umaskini.


Naye mkuu wa kituo cha polisi Kanyigo, A/INSP Callistus Ngonyani, akizungumzia kuhusu usalama,amewataka wanandoa kumaliza kutoelewana au migogoro  yao mapema ili isikomae na kukua,na kuleta madhara kama inavyotokea watu kuua wenzi wao,kujiua na maafa mengi mengineyo kama inavyosikika kwenye vyombo vya habari,akitolea pia mfano wa kitongoji cha Nyarwiga,kijiji Kashenye,ambako familia moja(majina yanahifadhiwa),wanandoa walikuwa wamefikishana katika hali tete ya kutishiana maisha,na kuwa suala hilo limeshughulikiwa.


Amewataka pia kama kuna wanaomiliki Solana kinyume cha sheria kuzisalimisha mara moja ofisi ya kijiji au kituo cha polisi,na hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi yao.


Baadhi ya waliochaguliwa kufuatilia mpango wa TASAF kijijini hapo


Baadhi ya viongozi na maafisa ugani

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso