Boti ikiwa imebeba wahamiaji haramu
TAKRIBANI watu 34 wamefariki dunia baada ya boti iliyobeba wahamiaji haramu kuzama karibu na Syria huku ikiwa bado haijajulikana siku ambayo boti hiyo ilizama.
Taarifa hiyo imetolewa Septemba 22, 2022 na Shirika la Habari la Serikali la nchi hiyo na kueleza kuwa boti hiyo ilitoka na wahamiaji hao nchini Lebanon, Palestina na ilipokaribia na Syria ikazima.
Kwa upande wa Shirika la haki za binadamu la Syria linalofuatilia vita nchini humo limeripoti kwamba takribani wahamiaji 36 wakifariki dunia katika Bahari ya Mediterania baada ya boti hiyo iliyowabeba wahamiaji haramu iliyokuwa ikielekea Ulaya kuzama.
Wahamiaji haramu wengi wamekuwa wakifariki kila mwaka kutokana na kuzama ndani ya maji katika bahati ya Mediterania
Tukio jingine lilitokea nchini humo ni la zaidi ya watu 1800 kupoteza maisha yao wakati wakijaribu kuvuka bahari hiyo kwa ajili ya kwenda barani ulaya.
Matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini humo ambapo mwaka 2013 wahamiaji haramu 254 waliokuwa wakitoka Syria kwenda Misri waliokolewa baada ya kuzama kwenye maji.
Wahamiaji wengi haramu wamekuwa wakiokolewa katika bahari ya Mediterania
Maelfu ya wahamiaji haramu wameripotiwa kuhama barani Afrika na pia Mashariki ya Kati na kuhamia barani Ulaya kila mwaka.
Wahamiaji wengi wanatumia mashua ndogo na kufunga safari ya kuelekea Bara la Ulaya kwa kupitia bahari ya Mediterania.
Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao
No comments:
Post a Comment