TOZO KUSITISHWA KUSABABISHA CHAI NA VITAFUNWA VYA VIONGOZI KUKATWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 20 September 2022

TOZO KUSITISHWA KUSABABISHA CHAI NA VITAFUNWA VYA VIONGOZI KUKATWA

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemuagiza mlipaji Mkuu wa Serikali kukaa na maafisa masuuli wote ili kuyaangalia upya mafungu ya matumizi mengineyo ndani ya serikali ili miradi yote ya maendeleo isiathirike, ikiwemo kukata kwenye chai na vitafunwa vya viongozi.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 20, 2022, Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu malalamiko ya watanzania kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki


"Ni dhahiri kwamba punguzo hili (Tozo kufutwa) litapunguza mapato ya serikali ninaelekeza fedha hizi zifidiwe kutoka kwenye kubana matumizi mengineyo ndani ya serikali ambayo hayataathiri utekelezaji wa majukumu ya msingi ya mafungu husika," amesema Waziri Nchemba


Aidha Waziri Nchemba akaongeza, "Tutafute maeneo tukate kwenye chai , vitafunwa, misafara kwenye safari za ndani na nje kweny wizara zetu, tukate mafunzo ya semina, matamasha, warsha makundi yanayokwenda kugkagua miradi ile ile yanakwenda makundi tofauti taofauti ,".

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso