Karibu watu watatu wamekufa baada ya tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.6- katika vipimo vya richta kuupiga mji wa Wau, New Papua Guinea mapema hii leo.
Kulingana na mamlaka watu wengine wamejeruhiwa na miundombinu imeharibika vibaya kutokana na tetemeko hilo.
Watu hao watatu wamekufa kwenye maporomoko ya udongo katika mgodi wa dhahabu wa mji huo wa Wau, hii ikiwa ni kulingana na mkurugenzi wa majanga wa jimbo la Morobe Charley Masange.
Ameliambia shirika la habari la AP kwamba watu waliojeruhiwa waliangukiwa na vifusi vya udongo na kuongeza kuwa baadhi ya vituo vya afya, nyumba na barabara ndogo na kubwa viliharibiwa.
Taifa hilo la kisiwa liliwahi kukumbwa na tetemeko kubwa la kipimo cha 7.5 mwaka 2018 na kusababisha vifo vya watu 125.
Chanzo:DW
No comments:
Post a Comment