Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainabu Telack
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainabu Telack, ameamuru kurejeshwa kazini mwalimu wa shule ya msingi Mtende, Halmashauti ya wilaya ya Kilwa, Stanley Ngaiza, aliyefukuzwa kwa madai ya utoro kazini kwa siku 11.
Mkuu huyo ametoa amri hiyo, baada ya kupokea taarifa ya masikitisho kutoka kwa Katibu wa Chama cha Walimu (CWT), wilaya ya Kilwa, Hamisi Bakari, kufuatia kutimuliwa kazi mwalimu Stanley Ngaiza, kwa utoro wa siku 11 kwa kosa linaloelezwa la kubambikiwa na uongozi wa (TSC) wilaya ya Kilwa.
"Jamani viongozi acheni kuonewa, watumishi mliopewa kuwaongoza, Lindi tuna upungufu wa watumishi, mnafukuzaje kazi kwa kosa lisilo lake?" alihoji RC Telack
Telack akitoa amri hiyo, amesema kitendo cha mwalimu huyo kufukuzwa kazi kwa kosa lisilo lake ni uonevu, hivyo akaamuru kurejeshwa mara moja kazini ili aweze kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kufundisha watoto.
Mwalimu Ngaiza amefukuzwa kazi mwezi Aprili mwaka huu,na kuelezwa tayari ameshakata rufaa mamlaka ya juu mkoani Dodoma kupinga uamuzi huo uliofanywa na TSC wilaya ya Kilwa.
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment