Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema, kutakuwa na upungufu wa mvua katika kipindi cha mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza Oktoba hadi Desemba 2022, zitakazosababisha kupungua kwa unyevunyevu katika udongo hivyo kuleta athari mbalimbali.
Imeelezwa kutakuwa na vipindi virefu vya ukame na kuna uwezekano wa kutokea kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ambayo inaweza kuleta athari.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa, Septemba 3, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka TMA, Dk Agnes Kijazi wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za vuli kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba.
Amesema hali hiyo inasababishwa na migandamizo midogo ya hewa ambayo imeendelea kuwepo katika ukanda mvua maeneo ya Somalia na hivyo kutarajiwa kuchelewa kwa mvua za vuli nchini.
Amesema migandamizo hiyo inatarajiwa kuanza kupotea ifikapo Desemba 2022 na hapo ndipo mvua kubwa zitaanza kunyesha nchini.
No comments:
Post a Comment