Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa nane [08] kwa tuhuma za kuharibu mali, kubomoa nyumba ya LUCIA BROWN KASEBELE [50] Mkazi wa Ibula wilaya ya Rungwe yenye thamani ya Tshs.2,500,000/=.
Watuhumiwa waliokamatwa ni:-LUPAKISYE MWANJISI [40] Mkazi wa Igogwe.
NELSON ANDRUM MWAKYEJA [34] Medical Record
LUSEKELO JOHAN MPANGATA [24]
MANENO ATHUMAN NDABILI [31]
SEMENI LUCKY [37]
ABEL WACHAWASEME MWAISUMO [42]
FANUEL PETER [39]
DAVES FONI [22] wote wakazi wa Ibula.
Ni kwamba Septemba 25, 2022 majira ya saa 03:30 asubuhi huko Kitongoji cha ibula, Kijiji cha ibula, kata ya kiwira, wilaya ya rungwe, LUCIA BROWN KASEBELE [50] alibomolewa nyumba yake yenye thamani ya Tshs.2,500,000/= na kikundi cha watu wa kitongoji hicho kutokana na kumtuhumu kuwa ni mchawi kwamba amemloga ELIKACHI MWAMBUNGU ambaye alifariki Septemba 21, 2022 kwa ugonjwa wa kichwa.
Watuhumiwa wote nane Septemba 26, 2022 walifikishwa mahakama ya Wilaya ya Rungwe CC.NO.84/2022 na kupelekwa Gereza la mahabusu Tukuyu. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kuwasaka balozi wa mtaa pamoja na mwenyekiti wa kitongoji ambao wamekimbia.
MTENDAJI WA KIJIJI AKAMATWA KWA TUHUMA YA MAUAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtendaji wa Kijiji cha Sangambi Wilaya ya Chunya JOSEPH NANGALE [45] kwa tuhuma ya mauaji ya kijana ARON MBUBA [18] Mkazi wa Kijiji cha Chalangwa Wilaya ya Chunya kwa kumpiga kwa kitu butu kichwani.
Ni kwamba awali Septemba 17, 2022 huko Kijiji cha Sangambi Mtendaji wa Kijiji hicho JOSEPH NANGALE [45] akiwa ameongozana na askari mgambo wawili wa Kijiji walimkamata ARON MBUBA [18] wakati wakikamata wauza mkaa ambao kazi hiyo bila kulipa ushuru wa Kijiji na pindi walipomtaka kulipa ushuru aliwajibu “hana hela” ndipo mtendaji wa Kijiji na Askari Mgambo walimpiga sehemu mbalimbali za mwili na baadae kumuweka mahabusu ya Kijiji hadi Septemba 19, 2022 baada ya kudhaminiwa majira ya jioni.
Akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Zahanati ya Kijiji cha Sangambi Septemba 20, 2022 majira ya saa 05:00 asubuhi ARON MBUBA [18] alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kupigwa.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kuwasaka watuhumiwa – Askari wa Jeshi la Akiba @ Mgambo ambao walikimbia mara baada ya tukio hilo. Aidha nitumie nafasi hii kutoa rai kwa wananchi na viongozi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapowakamata watuhumiwa kwa tuhuma mbalimbali na badala yake wajenge tabia ya kuwafikisha kwenye mamlaka husika ikiwa ni pamoja na vituo vya Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
Imetolewa na,
ACP Benjamin E. Kuzaga,
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya.
No comments:
Post a Comment