Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa ametoa siku 14 kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr Hassan Abbas kukutana na Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kutathimini mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars).
Agizo hilo la Waziri Mchengerwa limetokana na mwenendo mbaya wa Stars ambayo imekuwa nayo kwenye mashindano ya hivi karibuni ambapo wiki iliyopita iliondoshwa kwenye michuano ya wachezaji wa ndani CHAN na Uganda kwa jumla ya magoli 4-0
Katika hatua nyingine ameitaka BMT kufuatilia kwa kina pambano la Bondia Mtanzania Hassani Mwakinyo dhidi ya Bondia Muingereza Liam Smith lililofanyika mjini Liverpool kwani Serikali haipo tayari kuona sintofahamu ya mazingira yoyote kwa mwanamichezo wa kitanzania
Ilhali pia Waziri Mchengerwa ametaka kufanyika kwa mabadiliko kwenye kurugenzi za michezo ili kupata watu wenye kiu na wachapakazi watakaosaidia kuendeleza michezo hapa nchini huku ripoti kuhusu Taifa Stars ikitakiwa kuwasilishwa ndani ya siku 14
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment