MANISPAA YA TEMEKE YABAINIKA KUWA NA IDADI KUBWA YA WAGONJWA SURUA SERIKALI IKITANGAZA MLIPUKO WA UGONJWA HUO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 15 September 2022

MANISPAA YA TEMEKE YABAINIKA KUWA NA IDADI KUBWA YA WAGONJWA SURUA SERIKALI IKITANGAZA MLIPUKO WA UGONJWA HUO



Wizara ya Afya imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa surua katika halmashauri saba nchini huku watu 38 wakithibitika kuwa na ugonjwa huo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Alhamisi Septemba 15,2022 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amezitaja halmashauri hizo kuwa ni Bukoba yenye sampuli tatu, Wilaya ya Handeni sampuli nne, Kilindi tatu, Mkuranga nne, Kigamboni nane, Manispaa ya Temeke 12 na Manispaa ya Ilala nne.


“Mlipuko wa ugonjwa wa surua huthibitika baada ya sampuli tano za wahisiwa huchukuliwa kutoka wilaya moja ndani ya mwezi mmoja endapo sampuli tatu au zaidi kati ya hizo tano zilizochukuliwa zimetoa majibu chanya,” amesema Waziri Ummy.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso