Binti mmoja mwenye umri wa 21 anayejulikana kwa jina la Rehema Musa mkazi wa Mtaa wa Ilindi Kata ya Zongomera wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ambaye ni mlemavu wa viungo vya mwili anapitia changamoto nyingi baada ya kutelekezwa na Baba yake Mzazi zaidi ya miaka 20
Na Naomi Kidunu - Huheso Digital Blog
Akizungumza na Huheso Digital Tv Amina Imamu Kibila ambaye ni Mama mzazi wa Binti huyo Ameelezea kwa uchungu kuhusiana na changamoto ambazo anazipitia binti yake ambapo baadhi ya ndugu zake wamemtega mama huyo wakiamini kuwa ameleta mkosi kwenye ukoo wao
Mama mzazi wa binti huyo ameeleza kuwa anapata changamoto kubwa ya kumhudumia Binti yake maana yeye mwenyewe hana kipato chochote cha kukidhi mahitaji yake na anaishi katika mazingira magumu ikiwemo ukosekanaji wa mahali pa kuishi
Baadhi ya majirani wa eneo hilo Monica Richard na sande Buluba wamezungumzia Maisha halisi ya Binti huyo kuwa anapata shida sana maana hawezi kufanya kitu chochote Mfano kutembea, kuzungumza, kula, kufua, n.k
Kwa upande wake mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ilindi Ndg Dogo Mheziwa ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kuwatenga watu wenye ulemavu na kuondokana na imani potofu kuwa ulemavu siyo mkosi bali ni mpango wa Mungu jamii inatakiwa kuwajali na kuwapa nafasi
Ukiguswa na unahitaji kumsaidia tafadhali wasiliana na Mama Rehema kwa Namba 0753-367-865 na 0688-598-292.
Ukiitaji kumsaidia Rehema tafadhali namba zake hizo hapo juu pia unaweza kutuma Msaada wako kupitia akaunti
0150059582900 - Huheso CRDB bank
Pata muda uangalie masaibu anayopitia Rehema na Mama yake katika kumtunza baada ya kutelekezwa na Baba yake miaka 21 iliyopita.
No comments:
Post a Comment