Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeitaka Serikali kutoa taarifa ya sababu za hali mbaya ya kifedha iliyoutokea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), badala ya kukiri peke yake.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 20, 2022 na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salim Mwalimu Jumaa alipotoa maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichoketi Septemba 17 na 18 mwaka huu.
Mwalimu amesema kamati Kuu ya Chadema imeazimia kumuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya uchunguzi katika mfuko huo.
"Kamati Kuu imemtaka CAG kufanya ukaguzi maalumu kwenye mfuko huo na kujua mwenendo wa fedha za wananchama.
No comments:
Post a Comment