Na Kareny Masasy,
MKUU wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Festo Kiswaga amesema kuwa fedha za miamala ya tozo kiasi cha sh Millioni 537 .5 kilichopokelewa na halmashauri ya Msalala kimeweza kujenga miradi kwenye sekta ya afya na elimu.
Kiswaga amesema hayo leo tarehe 10/09/2022 alipofanya ziara ya kutembelea miradi hiyo ambayo imekamilika kwa asilimia 100 na mingine kuanza kufanya kazi.
Moja ya miradi aliyotembelewa ni shule ya sekondari Nyawile iliyopo kata ya Kashishi ambayo imejengwa vyumba viwili vya madarasa kwa fedha za tozo kiasi cha sh Millioni 25 nakuokoa wanafunzi kutembelea umbali wa zaidi ya kilomita 20.
Pia Kiswaga ameweza kutembelea kituo cha afya Mwalugulu kilichopo kwenye kata hiyo kilichotumia kiasi cha shilingi Millioni 500 kwa fedha za tozo ya miamala na ndani ya mwezi huu kitaanza kufanya kazi.
Makamu mkuu wa shule hiyo James Matiku amesema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 266 ilianzishwa mwaka 2021 ikiwa na vyumba vya madarasa viwili vilivyoanzishwa kwa nguvu za wananchi na sasa vyumba vya madarasa viko tisa vyote vimekamilika.
“Awali walikuwa wakisomea shule ya sekondari ya kata ya Bulige nakulazimika wanaoishi maeneo ya kata ya Kashishi kutembea umbali mrefu nakufikia wengine kutomaliza shule kwa kupata mimba na utoro wa rejareja lakini sasa hali hiyo haipo tena wanapata na muda wa kujisomea”amesema mwalimu Matiku.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Flora Sagasaga ambaye ndiye diwani wa kata ya Mwalugulu amesema kuwa anashukuru kuwepo fedha za tozo za miamala kwani zimewasaidia kupata kituo cha afya na majengo yote muhimu walikuwa na Zahanati pekee.
“ Wajawazito na watoto walikuwa wakiteseka kwenda Hopsitali ya manispaa ya Kahama kupata huduma umbali wa kilomita 30 hadi 40 lakini sasa watapata huduma hapa hapa kwani kuna jengo la wagonjwa wa nje (OPD)jengo la mama na mtoto,jengo la upasuaji,jengo la kuchomea taka na maabara”amesema Sagasaga.
Ofisa mipango wa halmashauri ya Msalala Elikare Zabron amesema kuwa wamepokea kiasi cha sh Millioni 537.5 kutoka serikalini fedha za tozo za miamala na ulifanyika mgawanyo sekta ya afya sh Millioni 500 na sekta ya elimu sh Millioni 37.5
‘Ambapo sh Millioni 25 zimejenga vyumba vya madarasa viwili Nyawile Sekondari,chumba kimoja sekondari ya Chela sh Millioni 12.5 na kituo cha afya kimoja cha Mwalugulu kiasi cha sh Millioni 500”amesema Zabron.
No comments:
Post a Comment