Charles III ametangazwa rasmi kama mfalme katika hafla ya kihistoria katika kasri la St James.
Bendera zilizoshushwa katika kumuomboleza Malkia, zitapandishwa juu kikamilifu baada ya hafla hiyo ya baraza la kumtangaza rasmi mfalme, hafla itakayopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni kwa mara ya kwanza.
Charles alipokea Ufalme punde tu baada ya kifo cha mamake Malkia Elizabeth II, lakini kikao rasmi cha kihistoria kilithibitisha jukumu lake Jumamosi. Baraza la kumtangaza rasmi Mfalme, kinachojumuisya wanasiasa wakuu, majaji na maafisa wengine walimtangaza rasmi kama mfalme. Ni mara ya kwanza hafla hii inapeperushwa kwenye televisheni.
Matangazo mengine yatatolewa rasmi kote Uingereza mpaka Jumapili, wakati bendera zitarudi kupepea nusu mlingoti.
Haya yanajiri baada ya Mfalme kuahidi kumfuata, kipenzi mamake kujitolea maisha kuhudumia katika hotuba yake ya kwanza iliojaa huzuni.
Siku ya Ijumaa ameliambia taifa khusu huzuni mkubwa alio nao, kwa kumpoteza mamake, akisifia mzaha, ukarimu wake na ‘uwezo wake wa kuona wema katika kila mtu’.
Mfalame ameahidi kulitumikia taifa kwa uwajibikaji usiotetereka kama aliokuwa nao mamake Malkia katika utawala wake wa miaka 70.
Charles alikuwa mfalme punde tu mama yake alipofariki, lakini baraza hilo la wakuu wanaomtangaza rasmi hufanyika ounde baada ya kifo cha mfalme kutoa tangazo hilo la mrithi wa kiti cha enzi.
Katika baraza hilo Mfalme atatoa tangazo binafsi kuhusu kifo cha Malkia na kula kiapo kulihifadhi kanisa la Uskotchi – kwasababu kuna mgawanyiko wa sheria kati ya kanisa na serikali.
Miongoni mwa watakaohudhuria hafla hii ni Camilla, mkewe Charles waliooana kwa miaka 17 mpaka sasa ambaye sasa amepokea wadhifa wa Malkia mkewe mfalme, na mwanamfalme mpya wa Wales, William.
Tangazo la kwanza linatarajiwa kutolewa katika roshani ya Friar Court ya kasri la St. James mjini London saa tano saa za huko, muda unaoambatana na mbwembwe za wapiga tarumbeta, milio ya bunduki zinazofyetuliwa kwa heshima katika bustani ya Hyde na katika Jumba refu maarufu la London Tower.
Licha ya kwamba sio sehemu ya shughuli hiyo rasmi ya kutangazwa mfalme, maneno "Malkia amefariki, Mflame aishi Maisha marefu" mara nyingi hutamkwa baada ya hapo.
Siku ya Ijumaa, Charles alikutana na umati wa watu waliopiga kelele "God save the King!" yaani Mungu mlinde Mfalme wakati akisalimiana na umati uliokuwepo nje ya kasri la Buckingham.
Baada yah apo alitoa hotuba kwenye televisheni akieleza matumaini kwamba Mwanawe William kama Mwanamfalme mpya wa Wales na mkewe Catherine - "wataendelea kuwatia watu moyo na kuongoza mdahalo wa kitaifa".
Kutawazwa kwa mfalme kutafanyika katika jini la London la Royal Exchange, kwani mama yake alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 70
Tangazo la kwanza linatarajiwa kutolewa katika roshani ya Friar Court ya kasri la St. James mjini London saa tano saa za huko, muda unaoambatana na mbwembwe za wapiga tarumbeta, milio ya bunduki zinazofyetuliwa kwa heshima katika bustani ya Hyde na katika Jumba refu maarufu la London Tower.
Licha ya kwamba sio sehemu ya shughuli hiyo rasmi ya kutangazwa mfalme, maneno "Malkia amefariki, Mflame aishi Maisha marefu" mara nyingi hutamkwa baada ya hapo.
Siku ya Ijumaa, Charles alikutana na umati wa watu waliopiga kelele "God save the King!" yaani Mungu mlinde Mfalme wakati akisalimiana na umati uliokuwepo nje ya kasri la Buckingham.
Baada yah apo alitoa hotuba kwenye televisheni akieleza matumaini kwamba Mwanawe William kama Mwanamfalme mpya wa Wales na mkewe Catherine - "wataendelea kuwatia watu moyo na kuongoza mdahalo wa kitaifa".
Matukio ya leo:
Baraza la kumtangaza Mfalme, hafla rasmi kumtangaza Charles kama mfalme litafanyinka 10:00 BST
Kuanzia saa tano, saa za London, Bendera zitapepea kikamilifu na kufuatwa kwa milio ya bunduki zilizofyetuliwa kwa heshima Matangazo ya ziada yatatolewa kutoka roshani ya kasri la St James na mjini London
Maafisa wakuu serikali watakula kiapo cha Mfalme Charles III katika bunge la wawakilishi
Ameelezea "mapenzi yake kwa Harry na Meghan" na kupongeza mkewe Malkia Camilla kwa " uwajibika imara kwa majukumu ".
Mfalme amekiri kuwa Maisha yake yamebadilika sasa, akieleza kuwa hatoweza kutoa "muda zaidi na nguvu" kwa wakfu mbali mbali na masuala ambayo alitoa usaidizi kwa miongo kadhaa kama mrithi wa kiti cha enzi.
Nini hufanyika katika baraza la kumtangaza Mfalme?
Kihistoria, hafla hii huhudhuriwa na baraza la washauri wa ufalme ambalo limekuwepo tangu enzi la wafalme wa Norman. Wakati wanabaraza wakiwa ni 700, wengi wakiwa ni wanasiasa wa zamani na wa sasa, ni wanabaraza 200 pekee watakaokusanyika.
Awali wanakusanyika katika kasri la St James pasi mfalme kuwepo. Mbunge wa chama cha Conservative Penny Mordaunt, aliyeteuliwa kuwa rais wa baraza na Waziri mkuu Liz Truss, atatangaza kifo cha Malkia.
Karani wa baraza hilo atasoma tangazo rasmi la Mfalme akijumuisha jina la Charles kwamba ndiye anayepokea wadhifa wa Mfalme – ambaye tunayemfahamu kama Charles III.
Tangazo hilo linatiwa Saini na kundi akiwemo mkewe mfalme, Mwanamfalme wa Wales na askofu mkuu wa Canterbury, kiongozi mkuu bungeni, askofu mkuu wa York na Waziri mkuu.
Rais wa baraza ataomba ukimya na kisha asome ratiba ya shughuli zilizosalia, akishughulikia matangazo ya umma na amri za ufeytuaji bunduki kutoa heshima katika bustani ya Hyde na jumba refu maarufu la London Tower.
Mfalme anaingia katika awamu ya pili ya baraza hilo linalohudhuriwa na wanabaraza wakuu na kutoa tangazo binafsi kuhusu kifo cha Malkia.
Anakula kiapo kulihifadhi kanisa la Uskotchi na kusaini nyaraka mbili ili kunakili, huku Malkia mkewe na mwanamfalme wa Wales wakishuhudia. Wanabaraza wakuu watasaini tangazo hilo huku wakiondoka.
CHANZO: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment