Afisa Ustawi wa Jamii wa Jiji la Dar es Salaam, Joyce Maketa, amesema kwamba miongoni mwa mambo yanayovuruga ndoa hadi kupelekea wanandoa kuachana inasababishwa na wanaume kuomba mahusiano kinyume na maumbile.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 6, 2022, jijini Dar es Salaam, kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio mara baada ya taarifa kuonesha kwamba kila mwezi ndani ya jiji la Dar es Salaam takribani ndoa 300 zinavunjika.
"Kumekuwa na mahusiano mapya (Kwa wanandoa) yanayopelekea wakati mwingine kuomba kuwa na mahusiano kinyume na maumbile hicho kimekuwa ni moja ya kitu ambacho kimekuwa kikivuruga ndoa nyingi na watu mwisho kuachana, tuachane na hizo tabia tunazozi-copy na tuishi maisha yanayompendeza Mungu," amesema Joyce
Aidha Joyce amezitaja baadhi ya sababu zingine, ikiwemo wanandoa kutaka mambo ya usasa tofauti na walivyolelewa, kuwa na matarajio na kutamani wayaishi maisha kama wanayoyaona kwenye filamu pamoja na mmomonyoko wa maadili, na kwamba tabia za wanandoa haziko sawasawa na ndoa za miaka ya nyuma.
CHANZO: EATV
No comments:
Post a Comment