MKOA WA KAGERA WAZINDUA PROGRAMU JUMUISHI YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 10 September 2022

MKOA WA KAGERA WAZINDUA PROGRAMU JUMUISHI YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO


Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Albert Chalamila,akikata utepe  kwenye Kitabu cha PJT-MMMAM  kwenye hafla ya uzinduzi, akiwa na wanafunzi wa darasa la awali shule ya msingi Rumuli, manispaa ya Bukoba. Anayepiga makofi ni Katibu Tawala wa mkoa, Toba Nguvila


MKUU wa Mkoa wa Kagera;Albert Chalamila ameizindua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto(PJT-MMMAM),mbele ya wadau wa maendeleo zaidi ya mia tatu,akiwahimiza wazazi na walezi kuwapa mazingira sahihi yanayohitajika katika malezi timilifu ili twaweza kukua  wakiwa na uwezo wa kujitegemea  na kutumainiwa na taifa lao.


Na Mutayoba Arbogast, Huheso Digital,Bukoba

 
Programu hii inawalenga watoto wa miaka 0 hadi nane  ambacho ni kipindi cha UJIFUNZAJI wa awali.


Amekemea vikali tabia za utoaji mimba na kutupa watoto kuwa hiyo ni laana mbele ya Mungu,na kuwa mtu akishaamua kushika mimba anao wajibu mkubwa katika matunzo ya mimba na mtoto,bila kwa kiasi kikubwa kumtegemea mwenzake,na kuwa hiyo haihalalishi kumtupa mtoto kwa sababu ya kutopewa matunzo na mwenza.


Wakitoa maoni yao na ushauri wakati wa uzinduzi huo,baadhi ya wananchi na viongozi wameshauri mambo mbalimbali,wakiwemo Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu ambaye amewaoya watu wajanja wajanja wasijipenyeze katika programu hii kwa lengo la kupiga pesa,na kukwamisha jitihada za kuwanufaisha watoto.


Bibi Agnes Mukuta (80), kutoka wilaya ya Biharamulo,amesisitiza usafl wa miili kwa wazazi ili kuepuka magonjwa yanayoweza kuzuilika,na hivyo kutowaathiri watoto wakiwa tumboni.


"Nashangaa kusikia ati UTI(Unirary Track Infection,yaani maambukizi kwenye mfumo wa mkojo) ni ugonjwa.Hapana ni uchafu.Mtu unamaliza haja yako ndogo wala hujipangusi,unakurupuka kufunga zipu ya suruali au sketi!!",amesema Bibi Mukuta.


Filbert Bandihai,mwenye ulemavu wa macho  na ambaye ni
makamu mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye Ulemavu Tanzania  (SHIVYAWATA)  halmashauri ya Bukoba,anesisitiza kuwa uangalizi usiwe kwa watoto wa kike tu bali pia kwa wavulana kwani sasa ndio wanasikika kuwa 'Panya road',lakini huwasikii wasichana.


“Kupitia programu hii itasaidia wazazi katika mkoa huu kuwa karibu sana na watoto wao ili  kufanya utambuzi wa watoto hao tangu wakiwa wachanga kama wanatatizo lolote, pia litakalosaidia watoto wenye ulemavu nao kujua haki zao za  msingi kama vile haki ya kupata elimu ili na wao waweze  kutimiza ndoto zao”,amesema Bandiahi.


Meneja mradi mtandao wa malezi, makuzi na Maendeleo ya watoto wadogo Tanzania(TECDEN), Lazaro Ernest,amesema kuwa,  kuna muongozo ambao  umeandaliwa na ofisi ya waziri mkuu  unaolenga katika utambuzi wa awali kwa watoto wenye ulemavu ambao utasambazwa katika mikoa yote ilikusisitiza suala la utambuzi wa watoto tangu wakiwa watoto.


Ameongeza kuwa mradi huu utatelezezwa kwa kipindi cha miaka mitano2021/22-2025/26 ukiwa na lengo la kudumisha makuzi, malezi na Maendeleo ya awali ya watoto nchini.


Naye Issa Mrimi,Afisa maendeleo mkoa wa Kagera,amesema mkoa unatarajia kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili kuieneza programu hii,kujenga uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwekeza kwa watoto,uanzishwaji wa kona za MMMAM,huku akisema wanaendekea kuomba kwa wadau na mashirika mbalimbali,na pia wakisubiri bajeti ya serikali,ili mkoa uweze kujenga vituo 81 vya malezi.


Jumla ya bajeti ya Programu Jumuishi kitaifa ni USD 394,392,824.


Bibi Agnes Mukuta kutoka wilaya ya Biharamulo akitoa nasaha zake


Filbert Bandihai,mwenye ulemavu wa macho akichangia maoni yake

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso