WAZAZI MKOANI KAGERA WAHIMIZWA KUTOA LISHE BORA KWA WATOTO KUIMARISHA UKUAJI WAO,NA UJIFUNZAJI WA AWALI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 7 September 2022

WAZAZI MKOANI KAGERA WAHIMIZWA KUTOA LISHE BORA KWA WATOTO KUIMARISHA UKUAJI WAO,NA UJIFUNZAJI WA AWALI


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh Albert Chalamila


MKUU wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amelishukuru shirika la Partage Tanzania linalomiliki Chuo cha Ualimu cha Partage Montessori kinachozalisha walimu wa Elimu ya Awali na Msingi,kuona pia umuhimu wa kutoa mafunzo kazini kuwawezesha walimu kupata ujuzi mpya katika eneo la ujifunzaji na ufundishaji.


Na Mutayoba Arbogast - Bukoba


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kazini kwa walimu wa Elimu ya Awali na Msingi Mkoani Kagera,ambayo yametolewa na shirika hilo,Chalamila amesema,pamoja na kuwafundisha mbinu za ufundishaji ni vema wazazi wakazingatia lishe kwani ukuaji wa mtoto unazingatia lishe ili mtoto aweze kuelewa yale anayojifunza na kufundishwa.


“Ni vizuri tukawa na mafunzo haya ya kuwapa walimu ujuzi mpya ili kuleta ufaulu mzuri kwa wanafunzi.Ukuaji wa mtoto una vitu vingi ikiwemo lishe.Lishe ndio muamuzi kwa watoto hawa,vinginevyo mnaweza mkakesha mnawafundisha lakini hawataelewa kama lishe zao si bora,hivyo katika hili nasisitiza katika agenda zetu za kudumu pamoja na kuwafundisha mbinu shirikishi za ufundishaji lakini tuone zaidi kwa wazazi lazima tuwalishe watoto hawa",ameeleza Chalamila.


Aidha,ameeleza kuwa ipo haja ya kuwafikia walimu wengi zaidi kwani ukilinganisha waliopata mafunzo na walimu ambao bado wanahitaji mafunzo hayo uhitaji bado ni mkubwa hivyo kuwaalika wadau wengine wa Elimu wenye nao wawezeshe mafunzo hayo kufanyika kwa lengo la kuinua hali ya ufaulu. Na kuwasihi wataalam kutoka Wizara ya Elimu na Wizara ya OR TAMISEMI kuwa na mikakati ya mafunzo kwa walimu yatakayosaidia kuinua ufaulu.


Afisa Elimu Mkoa wa Kagera, Ndg. Khalifa Shemahonge ameshukuru kwa mafunzo haya kuanzia Mkoa wa Kagera na kuwataka walimu wanaopata mafunzo hayo wajione kuwa ni mbegu hivyo walimu hao wanapandikizwa stadi za ufundishaji watakaporudi vituo vyao vya kazi wawe walimu wa walimu wenzao na kwenda kujikita katika kutatua changamoto ya tatizo kubwa ya kusoma,kuandika na kuhesabu.


Akisoma taarifa fupi, Bi Kemilembe Ndyamukama ameeleza kuwa, mafunzo haya yamelenga kuongeza ubora wa elimu inayotolewa kwani Elimu bora kwa vitendo itawawezesha watoto wa Tanzania kujikwamua kutoka katika maadui wakubwa ambao ni ujinga, maradhi na umaskini,na kuwa,kupitia mafunzo hayo,pia mtoto anaandaliwa mwenye kujitegemea, kuwa mwajibikaji, mzalendo na mwenye mapenzi mema na Taifa lake.


Mafunzo haya kwa kuanzia yametolewa kwa walimu 20 kwa uwakilishi wa kila Halmashauri.

Watoto wa Elimu ya Awali katika Chuo ualimu cha Partage Montessori

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalomiliki chuo cha ualimu cha Partage Montessori Phillip Krynen.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso