Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, ameitangaza mikoa mitano ambayo ipo hatarini kupata mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kuwa ni Kagera, Mwanza, Kigoma, Geita na mkoa wa Mara kufuatia mikoa hiyo kuwa karibu na wilaya ya Mubende nchini Uganda ambako ugonjwa wa Ebola upo.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Akizungumza hii leo Septemba 28, 2022, Waziri Ummy, ameitaja mikoa mingine ambayo amesema ipo kwenye tishio la kati la kupata mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kwa sababu ya kuwepo kwa viwanja vya ndege na vituo vikubwa vya mabasi kutoka nchi jirani kuwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Songwe, Mbeya na Dodoma na ametoa wito kwa wakuu wa mikoa yote nchini
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa serikali nchini Dkt Aifello Sichalwe, ameeleza mpango wa serikali kwenye kinga na hatua ambazo serikali inazichukua sambamba na kutoa wito kwa wananchi katika kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo.
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment