Watumishi wanne wa halmsahauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefukuzwa kazi baada ya kufanya uzembe na kumsababishia hasara mwajiri wao.
NA ERICK FELINO-HUHESO DIGITAL
Adhabu hiyo imetolewa na na kamati ya maadili ya madiwani wa halmsahauri ya Msalala baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wao watumishi hao.
Akisoma taarifa ya kamati hiyo iliyowakuta na hatia mbele ya Baraza la madiwani Jana, Agosti 16, 2022 mwenyekiti wa halmsahauri ya Msalala, Mibako Mabubu amesema watumishi hao wameisababishia hasara halmsahauri ya shilingi milioni 40 na kufanya kazi kwa uzembe.
Mabubu amesema waliofukuzwa kazi ni Edward Mnyoro ambaye ni mwekahazina, Dkt. Tanu Kilagwile Afisa mifugo, Shela Nazareti Afisa hesabu ambao wanadaiwa shilingi milioni 35 pamoja na Dkt. Mohamed wa zahanati ya Matinde ambaye yeye anadaiwa shilingi milioni 5.
Licha ya kufukuzwa kazi kwa watumishi hao bado wametakiwa warudishe fedha hizo na kama kuna mtumishi yeyote ambaye anaona atakuwa ameonewa anatakiwa akate rufaa.
No comments:
Post a Comment