Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dk Saada Mkuya amewasimamisha kazi wafanyakazi watano wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) wakiwemo wawili wanaodaiwa kushirikiana na wafanyabiashara kuchezea mfumo na kuisababishia bodi hasara ya Sh709 milioni.
Dk Saada akmemuagiza kamishna wa bodi hiyo, Yussuf Juma Mwenda kutekeleza agizo hilo mara moja na kuwachukulia hatua zaidi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (Zaeca).
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za bodi hiyo leo Ijumaa Agosti 12, 2022, Dk Saada amewataja wafanyakazi hao; Abdultif Abdalla Waziri na Kassim Idrissa Mussa wote kitengo cha Tehama ambao walichezea mfumo.
“Kamishna…, hawa watu kawasimamishe kazi kuanzia sasa halafu hatua zaidi za kisheria zichukuliwe kwa kushirikiana na Zaeca,” amesema Dk Saada
Wengine alioagiza wasimamishwe kazi ni mkuu wa kitengo cha Tehama, Harith Abdulaziz Ahmada; mkuu wa kitengo cha Madeni na Mapato, Asya Abdulsalam Hussein na meneja wa mifumo hiyo, Nassor Ali Juma na kubainisha kuwa haiwezekani watu wanaowasimamia wafanye mambo ya ovyo bila wao kujua.
No comments:
Post a Comment