Jumla ya mapipa ya lami 32 yenye thamani ya zaidi shilingi milioni 30, yamekamatwa wilayani Bunda mkoani Mara baada ya kuweka mtego na kubaini wezi ambao wanaiba vifaa pamoja na malighafi zinazotumika katika ujenzi wa barabara ya Buramba Nyamswa inayojengwa na kampuni ya CRCC ya nchini Chi
Akizungumza tukio hill Mkuu wa wilaya hiyo Joshua Nassari, amesema tabia ya wizi wa malighafi zinazotumika katika ujenzi wa miradi umekuwa ni wa mara kwa mara jambo ambalo lilipelekea kufanya uchunguzi wa kina na kubaini uwepo wa mtandao ambao unafanya uhalofu katika mradi huo.
"Niliamua kufanya mwenyewe uchunguzi huu kwa kuwashirikisha watu wachache ndipo juzi tarehe 23 usiku nilipokuja hapa katika pori hili na kukuta wizi ukifanyika," amesema Nassari.
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment