Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Kahama imetoa wito kwa wafanyabiashara kuwa na tabia ya kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka adhabu ya kutozwa faini na penati kutokana na kukiuka kanuni , taratibu na sheria za kodi.
Na Patrick Mabula ,Kahama.
Wito huo umetolewa jana na Meneja TRA msaidizi wa mkoa wa kikodi wa Kahama, Honest Mushi kwenye semina ya siku moja ya kutoa elimu ya mabadiliko ya kodi kwa mjibu wa sheria ya fedha kwa mwaka 2022 kwa wafanyabishara wilayani hapa.
Mushi aliwataka wafanyabishara kuwajibika kulipa kodi kwa wakati waweze kuepuka kupigwa penati na faini kwa mjibu wa sheria ya kodi kwa sababu adhabu hiyo wanapoilipa inatoka sehemu ya faida ambayo ni hasala kwao.
“Penati , faini na liba anayotozwa mfanyabiashara kwa kuchelewa kulipa kodi anapoilipa inamega sehemu ya faida yake ni hasala kwa hiyo wito wangu kwenu nawataka mbadilike na kuwa na tabia ya kulipa kodi kwa wakati,, Alisema Mushi.
Alisema suala la kulipa kodi lipo kwa mjibu wa sheria kati ya TRA na Mfanyabiashara kwa hiyo hakuna sababu ya kuwafanya wafanye biashara kwa hofu na kutokuwa na amani wanapaswa kutimiza wajibu wa kulipa kodi kwa wakati na furaha.
Mushi alisema katika kikao hicho amebaini bado kunachangamoto na malalamiko ya wafanyabiashara kwa sababu ya kutokuwa na uelewa wa elimu ya sheria za kodi kwa hiyo TRA itaendelea kuwaelimisha mara kwa mara kwa hiyo hawapaswi kukata tamaa.
Afisa TRA wa Idara ya elimu kwa mlipa kodi , Ancethi Kailagile utoaji elimu ya kodi kwa wafanyabiashara ni endelevu na kuwataka kuwa wanahudhulia pale waweze kuwa na uelewa wa sheria za kodi kutakako wasaidia kufanyabiashara kwa amani na furaha bila hofu.
Kwa upande wao wafanyabiashara Gifti Lwila na Godbether Felician waliitaka TRA kuendelea kuwapatia elimu ya sheria ya kodi iweze kuwasaidia kuepukana na adhabu ya kutozwa faini na penati kwa sababu ya kutokuwa na uelewa wa sheria na taratibu za kodi.
Mmoja wa Afisa TRA wa mkoa wa kikodi, Kahama Jaliwa Wilson akitoa mada ya elimu na mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka 2022 kwa wafanyabiashara wa wilaya ya Kahama iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kahama Picha na Patrick Mabula.
Wafanyabishara wa wilaya ya Kahama wakiwa kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kahama walipokuwa wakipewa elimu ya kodi na mabadiliko ya sheria zake iliyokuwa ikitolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) .Picha na Patrick Mabula.
Meneja msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa mkoa wa kikodi Kahama , Honest Mushi akitoa elimu ya kodi kwa wafanyabishara wa wilaya ya Kahama iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kahama,Picha na Patrick Mabula.
Afisa wa TRA wa kitengo cha elimu kwa mlipa kodi wa mkoa wa kikodi Kahama , Ancenth Kailagile akiongea kwenye semina ya siku moja ya kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabishara wa wilaya ya Kahama ,Picha na Patrick Mabula.
No comments:
Post a Comment