Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela amewaonya wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii kupotosha juu ya zoezi la Sensa kuacha kusambaza upotoshaji huo ili waweze kuepukana na mkono wa sheria wa makosa ya kimtandao unaoweza kuwafikisha mahakamani.
Shigela ameyasema hayo mara baada ya kumaliza zoezi ya kuhesabiwa lililofanyika nyumbani kwake asubuhi ya leo na kuwaasa wananchi waache upotoshaji huo.
"Ni vyema mwananchi usijiingize kwenye hilo tatizo kama kuna mwanachi ameposti hakuna sababu ha wewe kuendelea kuisambaza kwa sababu unapoisambaza na wewe unaingia kwenye hilo kosa la mtu wa kwanza alietengeneza ule uwongo kwenye zoezi lile la sensa, kwahyo ni kinyume cha sheria ni makosa kwa mujibu wa sheria zetu wanaweza kufikishwa mahakamani pamoja na kifungwa, ukiona taarifa kwenye group lako imepostiwa inayodhihaki zoezi la Sensa inayotoa taarifa za uhongo ni vizuri kiongozi wa group husika aweze kulifuta ili group lake liendelee kuwa salama", alisema Shigela.
Kwa upande wake mratibu wa Sensa mkoa wa Geita Khalid Msabaha amewatoa wasiwasi wakazi wa Geita kuwa wote watafikiwa na zoezi la Sensa kwani makarani zaidi ya 5000 kwa ajili ya zoezi hilo.
Via EATV
No comments:
Post a Comment