Shirika la Upelelezi wa ndani la Marekani, FBI limegundua nyaraka zenye siri nzito za serikali kutoka katika makaazi binafsi ya rais wa zamani Donald Trump, kulingana na hati zilizochapishwa jana na mahakama.
Maafisa wa FBI walichukua seti 11 za nyaraka wakati walipovamia na kufanya msako siku ya Jumatatu katika jumba binafsi la Trump la Mar-a-Lago mjini Florida.
Mbali na nyaraka zilizoainishwa kuwa siri za serikali, lakini pia kulikuwa na nyaraka ziliwekwa alama ya "siri nzito" ambazo zilikusudiwa kulinda siri muhimu za taifa na endapo zitawekwa hadharani zinaweza kusababisha athari kubwa kwa maslahi ya Marekani.
Maafisa wa FBI walikuwa wakichunguza uwezekano wa ukiukaji wa sheria tatu tofauti ikiwa ni pamoja na ile inayosimamia kukusanya, kusambaza au kupoteza taarifa za ulinzi chini ya Sheria ya Ujasusi.
chanzo: dw
No comments:
Post a Comment